Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Chipsi ni chakula kinachopendwa na watu wa rika zote.Ni moja ya vyakula maarufu sana Duniani.
Chipsi hupikwa na kuliwa katika namna mbambali,kwa kawaida huliwa na vyakula vyenye asili ya protini
kama nyama na mayai,Hata ivyo unaweza kula chipsi na mboga za majani.
Naamini wengi mmewahi sikia pishi la Chipsi masala,na pengine mmekula mara nyingi na mnafahamu
namna ya kuliandaa.Kawaida pishi hili huchanganya chipsi na mboga za majani katika kikaango na kuongezwa vionjo vya viungo mbalimbali.
Hapa jikoni napenda kufanya mambo tofauti ,Ubunifu jadi yangu.
Mahitaji.
Moja
- Mafuta ya majarini kwa kiasi upendacho (nashauri Blue Band)
- Vitunguu maji 3 vikubwa-kata kwa urefu
- Karoti 3 kubwa–kata vipande virefu Vyembamba
- Hoho 3 kubwa -kata vipande virefu vyembamba
- Vitunguu saumu vijiko 2 vya chakula-kata vipande vyembamba
- Carry powder kijiko 1 cha chai
- Chips masala vijiko 4 vya chai
- Pilipili manga ½ kijiko cha chai
Mbili
- Nyanya ya kopo-vijiko 3 vya chakula
- Giligiliani 1/2 kikombe –kata vipande vikubwa
- Sukari kijiji 1 cha chai
- Chumvi Robo kijiko cha chai
Tatu
- Maji nusu kikombe
Nne
- Kaanga chipsi
Njia
1.Katika sufuria,weka mahitaji yote ya namba moja.Tanguliza mafuta chini.Kaanga kwa moto mdogo adi karoti isinyae.
- Ukitumia moto mkali,viungo vitaungua kabla mboga hazijaiva
2.Ongeza viungo vyote vya namba mbili.kaanga pamoja uku ukichanganya adi uone nyanya na mboga vimeshikana na kua kitu kimoja
3.Ongeza maji nusu kikombe,changanya kisha acha vichemke kwa muda kidogo ili maji yapungue na kuacha mboga zikiwa na rojo zito
4.Kaanga chipsi
5.Weka chipsi kwenye sahani kisha weka mboga za chipsi masala juu yake.Tayari kwa kula
Maelezo ya ziada
Unaweza kutenga chaakula hiki kwa namna yoyote uipendayo.Hapa jikoni Niliamua kuweka juu ya jani la
sukuma wiki na kupamba na Tomato sosi.
Ukipenda kutenge hivyo.chukua jani la sukuma wiki,osha vizuri.Chemsha maji ya moto yanayotokota
kwenye sufuria pana, tumbukiza jani hilo kwa sekunde 25,kisha toa na ulitumbukize kwenye maji ya baridi
yenye barafu kwa sekunde 25.Toa kwenye maji,acha likauke au kausha kwa kutumia karatasi za
jikoni.Adihapo waweza litumia kutenga chakula.
- Lengo la kutumia sufuria pana ni kuhakikisha jani halijikunji
Kama familia ina watoto wadogodo,ni vyema ukakata mboga vipande vidogo,twanga au ponda vitunguu saumu na epuka kutumia pilipili manga.