Chogomundu Pangalashaba

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
Basi leo asubuhi nimemuona mrembo mzuri masikini hata hawezi kugombania gari, nikaona hapa hapa ndio pa kuchukua ujiko!

Nikapanda fasta nikawahi siti ya watu wawili halafu nikakaa katikati ili akija nimpishe, dah! Si likatokea libabu moja limevaa miwani kubwaa kama ya kukatia vitunguu likakaa! Duh linanuka tu sigara.

Yule Mrembo akasimama, moyo ukaniuma kweli!,
Daladala ilipofika Makumbusho nikaona lile Babu linashuka, aisee kama zali na Mrembo akakaa!

Jaman bahati iliyoje hii. Nikaanzisha story,
MIMI : Mambo Mrembo

MREMBO : poa,

MIMI : Karibu Karanga (nikatoa viujugu vya kuzugia)

MREMBO : silagi huo Uchafu,labda Pop Corn na Clips

MIMI : Ok naitwa Chogomundu Pangalashaba, siju mwenzangu?

MREMBO : He he heee! Jina kama dawa!, mi naitwa Princess Rihanna!,

Wakati naendelea kupata majibu Machungu ghafla Nikaona Gari imefika Namanga. Kwa kweli kama huyu mrembo angekuwa anatoa majibu ya kuridhisha ningeenda kushuka nae popote. Lakini kwa kuwa alishanikera nikamwambia konda "Shusha Namanga"

Sasa wakati nashuka nikashangaa kumbe na yeye anashuka hapo hapo!

MIMI : haa kumbe na wewe unashuka hapa?

YEYE : so what?

MIMI : ok umekataa karanga zangu, basi twende hapo kwa Mama ntilie tukagonge chai,andazi maharage,

YEYE : khaa! Unikome, mimi huwa natumia vitu kama Burger,Kuku, sausages,Pizza, Egg Chops na Chipsi Mayai. Yaani Uzuri Wangu wote unilishe kwa Mama ntilie? KOMA!,

Dah Mrembo akasepa zake, nikaona hakuna Noma, nikaingia zangu kwa mama ntilie nikaagiza Maharage ya 200,maandazi mawili 200 na Chai ya 100, nikaacha kajero hapo nikasepa.

Nimefika Kwa Shangazi akafurahi kweli kuniona.

SHANGAZI : mwanangu
Chogomundu Karibu Baba!,

MIMI: asante Shangazi

SHANGAZI: yule mwanangu wa Mwisho unamkumbuka?

MIMI : Si yule Kipandauso?

SHANGAZI: huyo huyo!

MIMI : namjua vizuri, wakati anakuwa namuona, hata nepi nimembadili teh! yupo wapi siku hizi?

SHANGAZI : amekuwa mkubwa kweli, anasoma Hapo Chuo Cha Kodi TRA pale karibu na ITV, ila alienda Chuo akahisi homa kaona arudi,ngoja nimuite.. Kipandausooooo!!!

KIPANDAUSO : beeee Mama!

SHANGAZI : Njoo mwanangu,kuna Mgeni!

Hamad! Ndipo Macho yangu
yakakutana na Yule Mrembo wa Kwenye daladala, kavaa vitenge vya zamani vya Shangazi, hana Wigi tena, muda huu komwe la ukoo linaonekana, komwe la babu yetu!,

Mrembo kashika sahani ya Maboga na kikombe cha uji wa Mchele!, Aliponiona Almanusura azimie!!!,

Huyu ndiye Kipandauso, Mtoto wa Mwisho wa Mjomba Dindoyogo!, ukipenda Muite Kipandauso Dindoyogo!

SHANGAZI : Njoo na Maboga ya kutosha na kikombe kingine cha uji uje unywe na Kaka yako!

Dah! akarudi ndani kinoma noma kainamisha sura chini. Ni nikawa najiuliza wapi Pizza? Wapi Burger? Wapi Sausage?,..

Anyway bado nipo hapa kwa
Shangazi mpaka baadae, nitakujuza litakalotokea.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…