Fungus inatokana na unyevunyevu ndani ya ukuta na kushindwa kutoka nje kwa urahisi. Huu unyevunyevu unaweza kuwa unatoka na maji kupanda ndani ya ukuta bila kizuizi kama hukuweka damp proof course na membrane.
Au unyevunyevu unaotokana na sehemu tunazoogea. Nyumbani hatuna kawaida ya ku waterproof mabafu yetu kwa kuamini kuwa tiles zinatosha. Tiles hazitoshi kwa sababu maji yanapenya kwenye maungio. Dawa ni kuweka waterproof membrane kwenye sakafu na kuta za bafu kabla ya kuweka tiles.
Kwa kuta za nje, badala ya kutumia rangi tulizozea tumia "masonry paint". Masonry paint inazuia maji kuingia wakati inaruhusu ukuta kupumua na hivyo unyevunyevu wowote unatoka nje ya kuta na unadondoka kama punje punje za maji.
Rangi ya weatherguard kwa nje inasaidia kwa kiasi fulani kuzuia fungus. Wash n wear haimudu hali ya nje.
Chokaa inaruhusu ukuta kupumua lakini kwa sababu sio waterproof itakubidi kuipaka mara kwa mara.
Kitu muhimu ni kuhakikisha kuwa nyumba yako haipenyezi maji. Aidha, hakikisha mabafu yanapata hewa fresh ya kutosha. Hakikisha paa halivuji.
Kitu kingine cha kuzingatia ni maintenance. Ukiona fungus zinajitokeza, ziondoe kwa kutumia dawa itakayoiua. Kagua kuta zako kila baada ya miaka mitano. Rangi zina muda wa kuwa effective.
Ongea na dealer wa rangi kwa ushauri zaidi. Au nenda hata kiwandani kwao ili upate ushauri.
Nakutakia kila la heri.
Amandla...
Masanja