Chokochoko Irani na Ufaransa!

Chokochoko Irani na Ufaransa!

Raphael Thedomiri

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2019
Posts
442
Reaction score
729
Iran iliionya Ufaransa Jumatano baada ya jarida la kejeli la Charlie Hebdo kuchapisha katuni zinazomoonyesha kiongozi mkuu Ayatollah Ali Khamenei ambazo Tehran iliziona kuwa za kashfa.

Jarida hilo la kila wiki lilichapisha katuni kadhaa za kumkejeli kiongozi huyo wa juu kabisa wa kidini na kisiasa katika jamhuri ya Kiislamu kama sehemu ya shindano lililoanzishwa mwezi Disemba kuunga mkono vuguvugu la maandamano lililodumu kwa miezi mitatu.

"Kitendo cha matusi na aibu cha uchapishaji wa Kifaransa katika kuchapisha katuni dhidi ya mamlaka ya kidini na kisiasa hakitapita bila jibu," Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian aliandika katika ujumbe wa Twitter.

Baadaye Jumatano, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ilisema kuwa imemwita balozi wa Ufaransa Nicolas Roche.

VOA
 
Iran wanashindwa kujua kuwa France anachochea maandamano kimtindo ili Iran izidi kupotea
 
"Kitendo cha matusi na aibu cha uchapishaji wa Kifaransa katika kuchapisha katuni dhidi ya mamlaka ya kidini na kisiasa hakitapita bila jibu," Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian aliandika katika ujumbe wa Twitter.
Vibonzo aina hii viliwahi kusababisha shambulizi kwenye ofisi za hilo gazeti na wachoraji wake kuuawa, naona wameanza tena kuwachokoza wenye itikadi Kali.
 
Back
Top Bottom