Chomete akabidhi tofali 1,000 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya serikali ya mtaa

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433


Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Mhe. Ghati Zephania Chomete tarehe 05 Septemba, 2026 amekabidhi tofali elfu moja (1,000) kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya serikali ya mtaa wa Chomete, Kata ya Sabasaba katika Halmashauri ya Mji wa Tarime, Mkoani Mara.

Tofali hizo zimekabidhiwa na Mhe. Dorice Maxmillian Chacha - Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Tarime kwa niaba ya Mhe. Ghati Chomete akiwa ameambatana na Diwani wa Kata ya Sabasaba Mhe. Raymond Mwema pamoja na Mhe. Nuru Hotay - Diwani wa Viti Maalum.

Makabidhiano hayo pia yameshuhudiwa na Ndg. Neema Newland Chacha - Mjumbe wa Kamati ya Siasa na Mwenyekiti wa UWT Wilaya Tarime.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…