Chonde chonde CHADEMA, wasameheni wabunge wenu 19 wa viti maalumu kwa maslahi ya chama na taifa

Ushauli wako Mimi nimeupokea kwa Maslahi mapana ya Nchi lakini kabla ya Hilo kufanyika kwa nini usiwaase watawala waache kuumiza Tena watu?Mbowe kaumizwa kiuchumi na kimwili kwa kiasi kikubwa kipindi Cha JPM lakini amekuja mwingine nae anaendelea kumuumiza Tena Cha ajabu kwa kesi za kubambika,Sasa hapo Taifa litaponywaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili la Mbowe wengi wamelisemea, na kwakweli SSH amepotoka mno kwenye hili.

Naamini hiyo tarehe 20, haki itatendeka.
 
Kama wahusika hawajawahi kuomba msamaha wao wataanzia wapi?
Ndiyo maana nimewashauri wale 19, wao ni kama watoto kwa CDM, wasibishane na chama, wajishushe wayajenge na chama chao.
 
Absolutely.
 
Mmeingia kwenye mtego mkubwa sana. Sameheni mfanye siasa za Kibunge. Hamuoni mmepigwa pin mikutano ya kisiasa, si vyema mkafanya siasa za Kibunge badala ya kijipiga pin huko pia?

Huko bungeni ndio wabunge wa upinzani walikuwa wanatolewa na kufungiwa kila siku. Hata Cdm wasiporuhusiwa kufanya mikutano, tayari Cdm wanafaida ya kizazi kinachojitambua. Hata wafanyiwe hila vipi, bado uhalisia utawabeba. Hilo bunge unalosema ndio hilo liko gizani, hivyo tuko vizuri maana watabana lakini wataachia.
 
Kamanda Halima Mdee na wenzake kamwe hawawezi kurudi kwenye genge la kihalifu.
 
Ndiyo maana nimewashauri wale 19, wao ni kama watoto kwa CDM, wasibishane na chama, wajishushe wayajenge na chama chao.
Vyama vya umma haviendeshwi kwa msingi wa baba, mama na watoto.
 
Wabunge wenyewe unaosema wasamehewe ndio hawa ambao wanawatanguliza waume zao ccm
 
Siyo tu Chadema hata serikali inabidi iwe inasemehe saba mara sabini...
 
Wenye nchi ndivyo walivyokua wameamua sasa wewe shida yako vip.hivi unajua kwenye hii dunia bado kuna binadamu kwa akili zao na usomi wao bado hawatakagi kuamini kua madaraka na maisha ni vitu vya kupita na kuna muda vinapita bila maandalizi wala kutarajia.Siasa pamoja na kwamba ni ajira kama ilivyo soka ila kukiwa na siasa za kubishana kwa hoja kunakua na faida kubwa sana kwa nchi kuliko kua na nchi yenye siasa mfu.sasa kuna watu waliamua njia ya pili badala ya kwanza ndo maana yakatokea yote hayo.Leo siasa imegeuka kua uadui badala ya ajira na kichocheo cha ajira,uwajibikaji na chachu ya maendeleo.
 
Covid19 washaliwa vichwa ,waendelee kuwatumikia waliowapeleka bungeni.
 
Kamanda Halima Mdee alisha sema yeye ni Chadema hadi mwisho.
na ni wabunge halali wa chadema.
Unajielewa mwenyewe kwanza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…