Bwanawe!Kama unajua kuliko na siasa za ubabaishaji ni huko elimu ya msingi.Halmashauri za mitaa na vijiji ndio wasimamizi wa shule,walimu wakuu hawana chao kule.Diwani akiamua mratibu elimu hana chakushauri,kwa sasa maafisa elimu wa wilaya ni watumwa wa madiwani kila kitu "sawa mheshimiwa"akileta utaalamu wake anarudi kwenye chaki na wengi wanaogopa chaki kama ukoma.
Kwenye mtihani ya darasa la saba huko ndio basi kila siku ina boreshwa ili wanafunzi waweze kushinda na baada kuona wanashindwa hesabu sasa ni mtihani wa kuchagua.Maboresho mengi ni ya kisiasa zaidi.