Chonde chonde wamiliki wa vituo vya redio na luninga: Tuondolerni hao wachambuzi uchwara wa soka!

Chonde chonde wamiliki wa vituo vya redio na luninga: Tuondolerni hao wachambuzi uchwara wa soka!

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Nitoe wito kwa wamiliki wa vituo vya redio na luninga kuwa watuondolee mbali hao wachambuzi wa soka uchwara.
Kuna wachezaji kibao wa zamani ambao wangetuchambulia soka kwa kutumia weledi na Siyo ushabiki. Wapo kina Sunday Manara, Zamoyoni Mogela, Boniface Mkwasa na watu wa aina Yao waliowahi kucheza soka katika kiwango Cha juu. Hao ndio wangetufaa, wanatukosea Sana kutuwekea kina Geoff Leah nk!!
Jifunzeni kwa Tv na redio za huko majuu. Hakuna mchambuzi/Commentator ambaye hajawahi kucheza mpira katika kiwango Cha juu au kuwa kocha katika kiwango Cha juu!! Huwezi ukachambua soka kwa weledi Kama hujawahi kufundishwa soka na kucheza katika ngazi za juu!!!
 
Mimi naomba waondoe ile wanaita Michongo pesa, sijui mshindo milionea and the likes

Naona Radio zote siku hizi zimeiga hii kitu, kipindi cha saa moja lakini nusu saa nzima wanapromote tu michongo pesa.
Hao ndo wanafanya kipindi kisikilizwe sasa sijui utawalipa mishahara wewe
 
Back
Top Bottom