Chonde chonde Zahera aondolewe mapema timu ya Yanga

Kalolelo

Senior Member
Joined
Oct 17, 2018
Posts
164
Reaction score
244
Tuseme ukweli na tuache unafiki Zahera timu imemshinda. Wengi watajivunia kumtoa Township Rollers lakini aina ya mpira tulioucheza ulikuwa mbovu sana ni bahati ilitokea na bahati huwa haijirudii mara mbili .
Pia najiuliza anataka apewe muda gani ili timu ifunge magori sasa kazi yake kama kocha ni nini. Kama pamba anamsumbua je ataziweza Azam, Mtibwa nk
Tumeanza na kichapo kwa ruvu shooting basi kuna vingine vinakuja vizito tukianza na Zesco, mbeya city, na prisons.
Nawaambia huyu jamaa kama hamjamfahamu hakosi sababu atakuja na sababu kibao mtaniambia muda utasema na viongozi mnamnyamaza
Ninaomba uzi huu baada ya Mechi hizo utumike kama rejea.
 
Mkuu mbn umekuja mbio mbio sana? Tuliza kwanza presha.
Tanzania imecheza leo na burundi na kashinda kupitia penalty
 
Mwinyi amewageuza Wana chura kuwa misukule.

Hizi hela anazotoa ni hongo shtukeni nyie wananchi,

Mtashuka daraja.

Timu inacheza Mpira usioeleweka, timu haifungi licha ya kuwa na mastriker maprofessional mnategemea nini??

Sisi wa unyamani tunafurahiiii Sana muendelee hivi hiviiiiiiiii.
 
Kwa namna Makamu Mwenyekiti anavyomtetea huyo Kocha, inaonekana bado yupo yupo sana mitaa ya Jangwani. Hivyo huna budi kumvumilia tu kama mimi.
 
yani unalinganishd mechi ya kirafiki ya pamba na mechi ya Zesco, Utakuwa na matatizo ya akili, wiki ijayo siyo mbali subiri uone zesco anavyoburuzwa
 
yani unalinganishd mechi ya kirafiki ya pamba na mechi ya Zesco, Utakuwa na matatizo ya akili, wiki ijayo siyo mbali subiri uone zesco anavyoburuzwa
Hv unawachukulia zesco poa yetu macho nimekwambia hata Mechi na roller ni bahat hakuna mpira tulocheza mwingi pia nakukumbusha hatugombani usitoe lugha chafu toa maoni na si kumwambia mtu kuwa hana akili ilikuwaje tukafungwa na ruvu shooting tatizo ukweli ukisemwa unakuwa mchungu kama hujui mimi ni Yanga Damu mpira unaonekana tunasema kinachoonekana
 
Naanza kuona mantiki ktk hoja yako. Anaejua anajua tu, mbona timu za taifa hupata muunganiko kwa haraka
 
Hapana hata na ruvu shooting mlikuwa mnajiandaa tu kwaajili ya zesco nyie wa kimataifa bhana,Mungu ajaalie mshuke daraja(jokes)
 
Nionavyo muda ndio utaongea na itakapobidi litafanyika hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…