Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Wakati joto la Uchaguzi Mkuu katika nafasi za Udiwani na Ubunge unaotarajiwa kufanyika hapo mwakani 2025 likiendelea kupanda, imeelezwa kuwa baadhi ya wanasiasa waliopo madarakani wameanza kupata shida kwenye maeneo yao kutokana na vigogo waliowahi kushika nafasi mbalimbali na wengine ambao bado wapo madarakani kuonekana kwenye majimbo ya uchaguzi hali inayopelekea wadau wa siasa kuamini kuwa kuonekana kwao ni kutokana na sababu ya kuhitaji nafasi za Ubunge.
Miongoni mwa viongozi wandamizi wanaotajwa kwa ukaribu ni pamoja na Mkuu wa mkoa wa Songwe na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Chama Cha Mapinduzi @ccmtanzania Daniel Chongolo aliyewahi kuwa Katibu mkuu wa CCM Taifa kuonekana kwa ukaribu mkoani Njombe na sababu kubwa ikitajwa ni kutokana na nia yake ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Makambako ili kumng'oa kigogo wa muda mrefu Deo Sanga maarufu kwa jina la (Jah People) ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa huo wa Njombe.
"Sina dhamira ya kuja hapa kutangaza nia yoyote, kwa sababu nimealikwa kwa dhamana ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wanaotaka tushirikiane kwenye maombi tushirikiane," amesema Chongolo