Chongolo: Stendi ya Chato iwe imekamilika mpaka kufikia Disemba 30, 2021

Chongolo: Stendi ya Chato iwe imekamilika mpaka kufikia Disemba 30, 2021

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amewaagiza Halmashauri ya Chato kukamilisha Ujenzi wa stendi katika Halmashuri hiyo ili kuwezesha wananchi kuingia na kuanza Biashara.

Katibu Mkuu Ndg. Chongolo ametoa agizo hilo leo tarehe 16 Novemba, 2021 wakati akiongea na viongozi wa mkoa na wilaya katika mkutano wa mapokezi uliyofanyika kwenye Halmashauri hiyo ambapo yeye pamoja na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashuri Kuu ya CCM Taifa wapo Mkoani Geita Kwa ziara ya siku mbili.

"Mimi niombe Halmashuri mmesema wenyewe hapa fedha yote ipo, Mimi nitarudi hapa tarehe 30 mwezi wa 12, Mambo yote kwenye hiyo stendi yawe yamekamilika, hatuwezi kuwa tunapiga makitaimu kwenye Jambo moja muda mrefu." Katibu Mkuu amesisitiza

Katibu Mkuu amesisitiza kuwa, lazima stendi hiyo ikamilike na kuwa historia ili wananchi waingia na kufanya biashara na Mambo yao yawanyokee.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu amewataka wanachama na wapenzi wa chama hicho kushawishi watu bora wagombee nafasi za uongozi ndani ya chama hicho katika uchaguzi Mkuu wa ndani ya Chama ambao unataajiwa kufanyika mwakani.

“Mwakani ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu wa Chama chetu, tafuteni watu bora na wazuri wenye uwezo na wenye dhamira ya kweli ya kuwatumikia wananchi wagombee nafasi ndani ya chama chetu."

Amewataka wananchi na wanachama wa CCM wasiache watu wasio na mapenzi mema kugombea nafasi hizo ndani ya chama kwa kutengeneza safu huku wakichagua wagombea kwa maslahi binafsi.

Katibu Mkuu Ndg. Chongolo ametoa wito huo wakati akiongea na wananchi katika mikutano ya mashina ambayo imefanyika Leo Wilaya ya Chato Mkoani Geita ambapo yeye pamoja na Wajumbe wengine wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wamewasili leo kufanya ziara ya siku mbili kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM pamoja na kuhimiza uhai wa Chama katika ngazi za mashina.

Imetolewa na;

Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
 
Hiyo stend yakujenga ndani ya siku 45 niya mtindo gani? Au kusembua nyasi.Haya maagizo ya uhandisi yasiwe kisiasa.
Hata haya madarasa ya uviko yatadondoka tu.
Hayamwagiliwi ipasavyo
Hayapumui
Matamkomatamko.
Rungu limeshikwa na wenyewe
 
Ila chato wangeacha kuifanya mkoa haitopendeza
Acha wapewe tu!Kuwapoza kwa lile pigo!!!jaribu kufikiria eti RAISI ALIEPO MADARAKANI ANATOKA KIJIJINI KWENU ANAFIA MADARAKANI!!!UNAOJE MKUU?SI KIOJA HICHO?KAGAME AMEUA WANGAPI NA BADO YUMO TU???
 
Acha wapewe tu!Kuwapoza kwa lile pigo!!!jaribu kufikiria eti RAISI ALIEPO MADARAKANI ANATOKA KIJIJINI KWENU ANAFIA MADARAKANI!!!UNAOJE MKUU?SI KIOJA HICHO?KAGAME AMEUA WANGAPI NA BADO YUMO TU???
Kweli inauma maana pengine ndicho kitu ambacho kilikuwa kinafanya kujivunia eneo utokalo
 
Back
Top Bottom