EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,477
- 15,325
Sare mpya za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zilizokamatwa nyumbani kwa Billionea huyo.
Moja ya tukio ambalo limewatikisa polisi baada ya kumkamata Mharami Mohamed Abadallah Chonji ni kumkuta na sare mpya za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) baada ya kufanya upekuzi wa kina nyumbani kwake Magomeni Kondoa, jijini Dar.
Sare hizo zinafanana kwa sehemu kubwa na zile zilizomwingiza Mbongo Fleva, Nasibu Abdul Diamond kwenye mzozo na jeshi hilo.
Mbali na sare kwa maana ya mavazi, pia mtuhumiwa huyo alikutwa na viatu vya jeshi hilo maarufu kwa jina la buti nazo zikiwa mpya!
Katika hali iliyowatia shaka zaidi askari ni pale Mharami alipopekuliwa zaidi na kukutwa na bastola ambayo jeshi la polisi halijaitolea ufafanuzi inaitwaje na ilitengenezwa nchi gani!
Vitu vingine vilivyokutwa kwa mtuhumiwa huyo ni jiko dogo la gesi na gundi ya plastiki, vyote vinaaminiwa kutumika wakati wa kutengeneza kete za unga tayari kwa kusafirisha.