Choo kinarudisha ndani kabla hata hakijatumika

The golden

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2018
Posts
1,382
Reaction score
2,582
Baada tu ya kuunganisha bomba kwenda kwenye Septic tank ,choo kilianza kurudisha harufu ndani, ikinyesha mvua ndio kabisa kinazidi . Fundi aliyetengeneza hapatikan

Lakini vyoo vingine vinavyotumia the same septic tank havirudishi ndani

Please, anayejua tatizo ni nini anaisadie.
 
Ametega vibaya/tenge kile ki u-shape . Kiufundi maji ndo yanazuia harufu isirudi. Ukitega vibaya Kuna space itabaki na harufu itakurudia.
Ni maoni yangu tu. Mimi sio fundi.
 
Ametega vibaya/tenge kile ki u-shape . Kiufundi maji ndo yanazuia harufu isirudi. Ukitega vibaya Kuna space itabaki na harufu itakurudia.
Ni maoni yangu tu. Mimi sio fundi.
Asante sana.
 
Mtag Mtaalamu akupatie consultation
 
Unatumia choo cha kukaa au kuchuchumaa (asian type)?

P/U-trap haijawekwa vizuri
 
P trap ikiwekwa vizuri, tatizo la choo kurudisha harufu ndani huwezi kukutana nalo. Hapo inawezekana kwenye maungio kati ya p- trap na bomba au p trap yenyewe kuna linkage (kunavuja maji), hivyo inafanya maji yapungue ama kuisha kabisa na kufanya harufu iweze kupita na kurudi chooni. Yale maji unayoyaona yanakaa kwenye p trap ndio yanayozuia njia ya harufu kurudi chooni
 
Asante mkuu.

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
 
Unatusumbua tu ungetafuta fundi mwingine sio kutuhangaisha. Eti fundi hapatikani, kwani una fundi mmoja utadhani mama mzazi
 
Ametega vibaya/tenge kile ki u-shape . Kiufundi maji ndo yanazuia harufu isirudi. Ukitega vibaya Kuna space itabaki na harufu itakurudia.
Ni maoni yangu tu. Mimi sio fundi.
Hili ndio jibu
 
Watanzania tupende kutumia wataalamu. Kutokutumia wataalamu hakukupunguzii gharama kunakuongezea gharama kama hii unayoipata leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…