Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,564
Tanzania ni Jamhuri, na ni muungano wa nchi 2, yaani Tanganyika na Zanzibar,kabla ya mwaka 1884, hapakuwa na historia ya nchi iliyoitwa Tanzania, isipokuwa zilikuwa ni tawala cha kichifu, kitemi kutegemeana na makabila ya maeneo mbali mbali yalipopatikana katika eneo ambalo hapo baadae liliitwa Tanganyika.
BERLIN CONFERENCE
(Mkutano wa Berlin) Nov 1884-Feb 1885
Mara baada ya mapinduzi makubwa ya viwanda huko ulaya na hasa kwenye miaka ya 1750, nchi ya Uingereza kufanya mapinduzi makubwa kwenye viwanda, na baadaye kwenye miaka ya 1850, mara baada ya kilichoitwa The great London Exhibition, nchi nyingi za ulaya ziliingia kwenye mashindano makubwa ya kiuchumi, na hasa kwenye upatikanaji wa mali ghafi pamoja na masoko, hivyo kupelekea kuwepo kwa migororo baina ya mataifa ya kibepari, kulikopelekea kutaka hata kusababisha vita miongoni mwao, na hatimaye aliyekuwa Chancellor, Bismarck wa Ujereumni kuamua kuitisha mkutano hapo Berlin ili kuondoa migongano na migogoro baina ya mataifa hayo ya ulaya. Mataifa mengi yali hudhuria, yakiwemo, Uingereza, Ujerumani, Italia, Ufaransa na mengine, Marekani na Dernmark yalihudhuria tu kama wasikilizaji, wao hawakuhitaji makoloni Afrika.
AFRIKA YAGAWANYWA MIONGONI MWA MATAIFA YA ULAYA
Wakati wa mkutano na mara baada ya kuichora ramani ya Afrika, mataifa haya ya ulaya yalikubaliana mambo matano ya kufanya ili kuwaepushia migogoro, mamabo hayo yalikuwa ni kama ifuatavyo: 1. Taifa lolote lililopata eneo Afrika, lilipaswa kuyajulisha mataifa mengine ya ulaya, 2. Kuweka mipaka,3. Kukomesha biashara ya utumwa 4.Uwandawa kongo kuwa chini ya King Leopard wa 2 wa Ubelgiji. 5. Mito yote mikubwa ya Afrika kuwa hruru kwa mataifa yote ya ulaya, kwaajili ya uvuvi na usafiri. Baada ya mgawanyo huu Tanganyika iliangukia mikononi mwa taifa la Ujerumani.
BAADA YA VITA VYA KWANZA VYA DUNIA 1914-1918
Mara baada kumalizika vita vya kwanza vya dunia, kwenye mkutano uliofanyika mwaka 1919 Lorraine Ufaransa, baada ya Ujerumani kukutwa na hatia ya kusababisha vita vya kwanza vya dunia, ilipewa adhabu kadhaa, zikiwemo, kulipa fidia ya athari za vita pamoja na kuachia makoloni, makoloni yote aliyokuwa akiyatawala, ikwemo Tanganyika, Cameroon, Togo, Rwanda na Burundi, aliamriwa kuyaachia.
Ikumbukwe kuwa, Ujerumani kama mkoloni, ndiye aliyefanya shughuli mbali mbali za kuindeleza Tanganyika kama Koloni Lake. Baada ya Tanganyika kuwa chini ya udhamini wa Baraza la umoja wa mataifa, Mwingereza akawa mwangalizi wake hakufanya chochote kwa kuiendeleza Tanganyika, badala yake alikuwa busy na makoloni yake kama vile Kenya, Uganda, Zimbabwe, Malawi, Zambia na mengine.
UCHUMI WA KIKOLONI TANGANYIKA
Uchumi wa kikoloni kwa sehemu kubwa ulitegemeana na upatikanaji wa malighafi na hali ya hewa ya eneo husika, Zaidi walifanya kilimo, uchimbaji wa madini na shughuli zingine, Kilimo walifanya Zaidi, Settler economy (Ulowezi) ma,
Plantation economy (mashamba makubwa huku wakiwa na wawakilishi tu kwenye maeneo hayo) na Peasant economy (kilimo cha jembe la mkono) ambacho waliwaachia wenye kufanya kilimo wenyewe na wao kununua mazao tu.
SETTLER ECONOMY(Ulowezi)
Aina hii ya uchumi wa kilimo kilifanyika Zaidi kwenye maeno ambayo hali ya hewa iliendana sana na maeneo wanayotoka wao, kama vile hali ya baridi, kama vile kwemye nchi za Kenya, Zimbabwe, maeneo haya waliyaendeleza sana, kwa vitu mbali mbali ikiwemo miundombinu mizuri, majengo, wakiamini kuwa wasingeondoka na badala yake wangeishi siku zote,
Na mara baada ya uhuru nchi hizi zilionekana kama kama vile zimepiga hatua sana za maendeleo, mfano wan chi hizi ni Afrika ya Kusini, hivyo hauwezi kabisa kulinganisha maendeleo ya Tanzania ambayo imejinga yenyewe na Afrika ya Kusini.
PLANTATION ECONOMY
(mashamba makubwa)
Aina hii ya uchumi ndio uliofanywa na Ujerumani hapa kwetu Tanganyika, ambapo wakoloni walikuwa na mashamba na huku wakiwa na wawakilishi tu, ambapo walikuja kuchukua mazao na malighafi zingine na kuzisafirisha kwenda kwao, huku wakiacha kuendeleza hapa Tanganyika, hata hivyo, walijenga miundo mbinu walau kidogo kama vile reli kuelekea kwenye maeneo ya kimkakati, kama vile kanda ya ziwa, kanda ya kaskazini na kuelekea Pwani. Hata hivyo Ujerumani hakudumu sana, baada ya kupokonywa koloni, kwaajili ya kusafirisha malighafi kwenda pwani, ili ziende Ulaya.
HARAKATI ZA UHURU NA BAADA YA UHURU
Mara baada ya vita vya pili vya dunia 1945, wakoloni walijua kabisa kuwa Waafrika wanahitaji kujikomboa, hivyo waliamua kuandaa mazingira ya kuitawala Afrika hata mara baada ya Afrika kujikomboa, waliamua kuandaa(Invisible governments) na viongozi vibaraka(puppet leaders)viongozi kadhaa waliandaliwa kuweza kushika madaraka baada ya wakoloni kuondoka lakini baade viongozi hao waligeuka na kuwa miiba kwa wakoloni hao na hatimaye kuamua kuwaua au kuwapindua kabisa, wakiwemo akina Patrice Lumumba, Mobutu Seseseko, Kamuzu Banda na wengine.
Hapa Tanzania zilianza zamani sana, wakati huo, Waafrika walinzisha migomo kadhaa ikiwemo kuanzisha vita dhidi ya Wajerumani walianzisha vita vya majimaji mwaka 1905-1907 katika kupinga uchumi wa kikoloni pamoja na suluba walizokuwa wakifanyiwa babu zetu.
KUANZISHWA KWA VYAMA VYA UKOMBOZI TANGANYIKA NA ZANZIBAR (1922-1977)
1922-hapa Tanganyika chama cha kwanza kuanzishwa kilianzishwa na Martin Kayamba, kiliitwa Tanyika Territory Civil Servant Association (TTCSA), kikiwa ni chama cha cha starehe, 1929 kilibadilishwa jina na kuitwa(Tanganyika African Association) TAA na hatimaye kikaamua kuhusika sana na kutetea maslahi ya wafanya kazi, 1954 mkutano mkuu Tabora, kilibadilishwa tena na kuitwa Tanganyika African Union (TANU), jina hili miongoni mwa majina mengi yaliyopendekezwa na wajumbe, lilipendekezwa na Bhogohe Makalanga, na Mwl.JK nyerere kuwa mwenyekiti wa chama cha TANU, chama hiki kiliamua sasa kuingia kwenye siasa za ukombozi wa TANGANIKA HURU chini ya uongozi wa Mwl.JK Nyerere baada ya kuamua kuachana na kazi yake ya ualimu rasmi mwaka 1955 pale Pugu.
Wakati wote wa harakati za ukombozi hapa Tanganyika kulikuwepo pia vyama vingine vya siasa, kama vile AMNUT, ANC chini ya Zuberi Mtemvu, lakini kwa sababu ya umahiri mkubwa na uongozi wa Mw.JK Nyerere, chama cha TANU ndicho kilifanikiwa kuikomboa Tanganyika kutoka kwa mkoloni Mwingereza 9-12-1961 na Mwl.JK Nyerere kuwa waziri mkuu na hatimaye 9-12-1962 kuwa Jamhuri na Mwl.JK Nyerere kuwa raisi wa kwanza wa Tanganyika, ilipofika mwaka 1965, kama taifa tuliamua kuwa na chama kimoja tu cha siasa ilikuweza kuongeza nguvu katika utendaji na ufanisi wa uwajibikaji kama taifa kwa kuisimamia vyema serikali.
CHANGAMOTO AMBAZO TUMEPITIA KAMA TAIFA
1967-1977-kuanzishwa kwa juamuia ya Afrika mashariki na hatimaye kuvunjika mwaka mwaka 1977, Tanzania ilipata hasara baada ya mali nyingi zilizokuwa mali za jumuia ya Afrika mashariki kubaki nchini Kenya, kama vile ndege zilizokuwa za jumuia ya Afrika mashariki na mashirika mbali mbali.
1978-1979-Tanzania pia ilingia kwenye mzozo mkubwa na Uganda, kati ya Mwl.JK Nyerere na Idd Amin aliyekuwa raisi wa Uganda kwa wakati huo, ambako pia kulipelekea vita baina ya mataifa haya mawili, ambapo nchi ilitumia raslimali nyingi sana na gharama kubwa sana katika vita hivi, miundo mbinu kuharibiwa ikiwemo madaraja,mfano daraja la kagera
1982-1992-SAP (Structural Adjustments Programmme)
Mkutano huu uliitishwa, Lagos Nigeria, ulikuwa katika ya World Bank (WB) International Monetary Fund (IMF) dhidi ya mataifa yanayo endelea, mkutano huu ulizungumzia mambo mengi sana lakini nitakugusia mambo mawili peke yake.
1. Subsidazation of costs (Wananchi kuchangia gharama za huduma za jamii), hapa mataifa yanayo endelea yaliambiwa na WB na IMF kuwa, kwa kuwa wana mzigo mkubwa wa madeni kutoka WB na IMF, hivyo hawakupaswa kuendelea kutoa huduma za jamii bure kama vile Elimu, afya na zinginezo, maana kwa Tanzania baada ya Azimio la Arusha la 1967, tulitangaza elimu kwa wote, Universal Primary Education (UPE) ya 1974, ambapo hata wasiojua kusoma na kuandika walipelekwa elimu ya ngumbalu.
2. Democratization process
(Mchakato wa demokrasia), ambapo waliatuambia tuanzishe Mult-Party system (mfumo wa vyama vingi) ikiwa na maana kuwa wasipopendezewa na chama kilichoko madarakani wanaweza kumuunga mkono mwingine, ili kuweza kuendelea kutimiza ukoloni mambo leo, na ndicho kinacho enedelea leo katika nchi nyingi za kiafrika, vyama vingi vya siasa vinapata ufadhili kutoka mataifa ya Ulaya.
MSTARI WA MBELE KATIKA KUPIGANIA UHURU WA NCHI ZA KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA
Mara baada ya Tanzania kujikomboa, Mwl.JK Nyerere alisema “Uhuru wa Tanganyika hautakuwa na maana kama hata nchi moja ya Afrika itaendelea kutawaliwa” hivyo basi tuliamua kuwa msatari wa mbele katika kupigania uhuru wan chi zingine za Afrika, na Tanzania ndiyo ilikuwa ndicho kitovu cha mapambano, tulitumia rasilimali nyingi katika kuwasaidia wenzetu, ambalo kwa hakiak lilikuwa jambo jema sana.
UKUBWA WA NCHI (Vastness)
Eneo lina kilometa za mraba 947,303 (nchi ya 31 duniani); maji ya ndani yanachukua ... Tanzania ni nchi kubwa zaidi kati ya wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. ... Nchi iko katika eneo la Maziwa makubwa ya Afrika, hivyo maziwa, hivyo ujenzi na undeleza wa miundombinu unahitaji muda wa kutosha na gharama kubwa sana ukilinganisha na nchi ndogo kama vile Rwanda.
USHAURI NA MAONI YANGU HASA KWA KWA VIJANA
Napenda kuchua nafasi, kuendelea kuipongeza nchi yangu na Serikali yangu kwa juhudi kubwa iliyofanywa tangu serikali ya awamu ya kwanza ya Baba wa Taifa Hayati Mwl.JK Nyerere, kwa maendeleo makubwa ya kimapinduzi, kwa kujenga Taifa lililo imara, lenye heshima kubwa ndani na nje ya Afrika
Tumejijengea mfumo bora na thabiti hata namna nzuri ya kuachiana madaraka, jambo ambalo ni mfano bora wa kuigwa kwa mataifa mengi duniani.
Ujenzi wa demokrasia na utawala bora, kuheshimia na kuvumiliana kisiasa, uendeshaji wa elimu ya siasa, dini, na jamii yenye mkusanyiko wa makabila mengi Zaidi ya 120, ni jambo la mfano ulimwenguni kote.
Maendeleo ya nchi, kwa kujenga miundo mbinu bora na kwa kujenga barabara, zilzojengwa nchi nzima, na washauri vijana, hasa hawa waliozaliwa miaka ya 90, huenda wanadhani nchi ilikuwa hivi kimaendeleo tangu tulipopata uhuru, huenda wanadhani hakuna hatua yoyote iliyofanyika.
Naomba wajue kuwa nchi hii imetoka mbali sana na itakwenda mbali sana, hasa kwa juhudi kubwa zinazo fanywa sasa na serkali hii ya wamu ya tano chini ya Jemedari mkuu Dr.JOHN POMBE MAGUFULI, mtu wa vitendo na kutekeleza anacho kiamini kwa ustawi wa taifa letu
Tanzania mpya inakuja
Daniel M. Kimbulu
Arusha Tanzania
0756 278 743
danielkimbulu@yahoo.com