Chris Lukosi katoa ushauri mzuri jinsi TRA wanavyokosa mapato

Gari jipya bei ya kununua iko juu lakini ushuru mdogo.
Gari chakavu bei ndogo lakini ushuru unatisha...hii ni kulipia uchakavu
Kwa Tanzania ushuru wa gari jipya (used la miaka ya karibuni) ni mkubwa zaidi kuliko ushuru wa gari la zamani la aina hiyohiyo. Yaani ushuru wa Toyota Mark X ya 2007 ni mdogo kuliko ushuru wa Toyota Mark X ya 2012. CiF walizojiwekea TRA kwenye kalkuleta yao ndio inaleta mahesabu kichaa ya hivyo
 
sahihi kabisa
 
Mambo yatabadilika tu maana tulilewa pombe imeshatutoka na sasa tumepata suruhu na iwe suruhu ya changamoto za kipumbavu zinazosababishwa na hawa walevi wanaoshindwa kufikiri vyema
 
Serikali ishaurike kwenye hili. Hawaoni wananchi wwnavyopata shida kwenye usafiri? Wanafikiri kujenga barabara, reli ndo kupunguza adha ya usafir?

Shusheni ushuru wa magari, watu wamiliki magari kwa bei nafuu uchumi utakua.

Wengi wanasema miundombinu yetu haiwezi kukidhi mahitaji, jamani kama mzee mwinyi asingetoa ruksa watu kununua magari pengine hata hizi flyovers zisingekua na magari.

Ruhusu magari ili utanue miundombinu, ndio ukuaji wenyewe huo.

Serikali punguzeni kodi, watu wanateseka na dalaladala, huko mikoani ndio kabisa Gari linaonekana anasa!
 
Tizama kodi ya toyota ist 2003 december na sasa


hapo kwa sasa kumbuka kodi wameshusha ist ya 2003 kuanzia January ilikua 6.2m ila sasa wameshusha kama 400k hv nme import ist ya mama watoto ya 2006 kwa kodi ya 6.6m ila sasa ni 6.2m. Kuna jamaa alinitonya tz ikikamilisha barabara zote na fly over folen itapungua na kodi zitashuka sana hvo tutaweza nunua hadi lamborghini[emoji23][emoji23]
 
Gari ya 2010 ushuru milioni 55!!! Sector ya usafirishaji bado ina safari ndefu sana Tanzania maana hiyo pesa hata south Afrika una nunua Mercedes Benz sprinter na change inabaki ya kuweza kununua Toyota quantum iliyochoka.

Nina rafiki yangu toka Malawi mwaka jana aliingiza horse 2 za MAN Diesel TGX pamoja na Iveco strallis za mid 2000,ametumia dola 2500 mpaka kuziweka road kule kwao. Kutajirika TZ ni hustle ndefu sana .
 
Bwana mdogo nipo hapa Helsinki,unapiga boksi wapi?
 
Bongo asilimia kubwa tunaendesha uchakavu wa kufa mtu bara zipo ila hazina magari watu wanaona kuna magari hapo...magari ya 2018 mengine kodi yanasoma 50m mengine 70m sijui wanafikiri nini watu hatuna magari ya safari mpaka lishikwe shikwe ndio utafute mkoa mwingine...punguzeni Kodi za magari sio chombo cha starehe kinachochea kukua kwa Uchumi mpaka gari za kubeba mchanga nazo Kodi zake zipo juu aisee..
 
wangeshusha ushuru wenye Ford ranger wangekuwa zaidi ya 500 na ushuru wangepokea zaidi na zaidi. Pia hapo hapo wauza spear wangeongezeka,
Mkuu sisi tunatakiwa kuishi kama mashetani, magari mazuri ni kwa ajili ya kina Bashite, Slowslow na yule KMK mstaafu ambaye sasa ni mbunge kiti maalumu.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
cha ajabu wajuba bado mna magari makali.

hapa ndio huwa naamini tanzania kuna watu wenye pesa wengi sana.

endapo watashusha hiyo kodi mambo yatakuwa poa zaidi.
 
Tiper usiguse ushuru wake ni balaa
 
Hili la kodi za magari haliitaji hata certificate nchi inapoteza kodi kwenye hii sekta au hata haiitaji huyo Lukosi muuza makinikia machakavu.Kuna kodi za kijinga sana nchi hii zisizokuwa na tija, sijui lack of exposure kwa baadhi ya watu waliopewa madaraka. Ndo maana hii nchi ni miongoni mwa nchi zenye watu wasio na furaha, serikali inawanyonga shingoni raia wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…