Christian Bella: Alipotoka Diamond muziki wa Bongo fleva ukaanza kuwa juu na muziki wa bendi kushuka

Tanzania kuna watu watatu katika bongo flava ambao naweza waita Kings kwa vigezo kabisa!!
Moja Joseph mbilinyi aka Sugu huyu alikomaa Sana na mziki enzi unaanza!!
mbili JosephHaule aka Prof Jay.. aliugeuza mziki kila mtu akaupenda
Tatu Nasib Abdul Juma aka Diamond platnumz huyu ameufanya biashara na kuupeleka mziki kimataifa na kuugeuza Kua pesa na ajira!! Wengine ni wasanii tu!!!
 
Mimi napenda sana muziki wa dance lakini hawa jamaaa hawana ubunifu na wanatunga minyimbo mingi inafanana.Christian anafanya vizuri lakini hawezi kudumu kwenye soko asipo team up na wakali wengine kama ilivyokuwa mwanzo.Wazee wa Ngwasuma nawakubali sana tangu waanze hawajawahi kuchemsha
 
Huyu kazaliwa jana?? Kunaambo mengi yaliua mziki wa dance hasa kuibuka kwa makundi kama tmk wanaume na Daz nundaz.. Hao wengine wamekuta game nyeupe ila wapongezwe tu kwa ku-maintain
 

kuddos to all bongo fleva artist ambao walikomaa enzi hizo wakati jamii iko chini ya miziki ya kikongo

wako wengi mno! maoni ya prof jay, sugu walibebwa hawa chini ya waliouanza, hao hawakuuanza

unataka shule?
 
Bela ana nyapianyapia tuu haujui mzik wa tanzania
 
Game limekua jeupe sana si kama wakati ule, hata Diamond, hiyo nyimbo yake iliyomtoa haikua Kali kivile ila ni kutokana na wakati tu. Ushindani hakuna tungo za maana hakuna basi ni kuishi ktk kwa kutegemea media tu, mkumbuke kua kipindi bongo fleva IPO katika ubora wake radio pekee ilitosha kuelezea ubora wa msanii.
 
Vipi wale vijana Yamoto band ?
Kasi yao imepungua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…