Christian Bella asema "Nagharamia" ukipewa airtime utakuwa mkubwa

Christian Bella asema "Nagharamia" ukipewa airtime utakuwa mkubwa

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Mkali wa masauti, Christian Bella amekiri wimbo wake mpya aliomshirikisha Alikiba ''Nagharamia'' haupo kwenye mzunguko mzuri kwenye redio kama ilivyotarajiwa na kwamba ukipewa airtime utakuwa mkubwa.

Akizungumza na Bongo5 leo, Bella alieleza sababu ya kwanini wimbo huo umeshindwa kufanya vizuri kama ilivyotarajiwa ukilinganisha na ukubwa wa wasanii waliomo.

Ngoma bado haina mzunguko kusema kweli, kwa sababu ilitambulishwa redio moja tu na bado haijakaa bado kwenye promotion,amesema.

Ngoma ni nzuri na itafanya vizuri, kwa sababu kuna ngoma nyingine inatambulishwa inafanya vizuri kwa siku za mwanzoni halafu inapotea lakini hii nina uhakika itafanya vizuri kutokana na muziki mzuri tulioimba.

Ngoja video itoke halafu watu wanajua nazungumzia nini kwa sababu mapokezi ni mazuri na watu wanahitaji kinachohitajika ni promotion tu.

Pia mimi wakati wimbo unatambulishwa sikuwepo, kwahiyo mimi naona ni promotion na wiki ijayo tunapokea video, aliongeza.

Chanzo: bongo5
 
umebuma licha ya kelele kibaooooooooooooooooooooooooooooo
 
Sasa wimbo umebumaje wewe kilaza??
 
Jamaa anatoa nyimbo nyingi kwa wkt mmoja, anaboa saa nyingine
 
Ninamuheshimu sana huyu mtu..

King of the best melodies,

Ila mmezidi uzembe upuuzi gani huo ahadi ya video inakuwepo afu kimyaa au mzee wa coming soon anamponza??? hata harmonize anawashinda??

Afu swala la promotion kwani ni lazima ufanye ukiwa bongo? ndio ubahili usiotakiwa huo, Diamond bongo ana managers kama wanne hivii, bado nchi za jirani anao ambassadors kazi ikitoka tu wao wanasambaza kazi vituo vikubwa UG, Rwanda, etc... Na wiki iliyopita kaongeza management baada ya kuingia mkataba na UPFRONT chini ya Mr Paulo mtu mkubwa sana Africa na huyo ndio atakuwa anammanage kwa upande wa west africa shows, endorsement deals, PR etc. na hiyo ndio bidii inayotakiwa kufanyika sio kubaki unapiga makelele tu mara oooooh nimegundua oooh wanatumia hela hahahahaha

Kama huwa unapitia huku BELLA OBAMA basi jiongeze, nakuaminia sana mkali wao... Ebu kaa chini na diamond akupe mikakati, kama ameweza kumfanya mtu aliyekuwa hajulikani kabisa, hana makazi maalum, kipato anatafuta kwa shida na muda mwingine akose hata nauli ya kwenda studio session mpaka apige debe ajaze gari ndio apande bure HARMONIZE, na kumfanya awe kati ya wanamuziki wanaofanya vizuri kwa sasa hadi kufikia kufanya video bora inayochezwa hadi MTV ambapo baadhi ya wasanii wakongwe bado mnaota siku mtakuja kuonekana, kwanini ashindwe kukupa support wewe?? ishu ya kusaidiwa ni kuonesha nia unataka msaada
 
Uzi kama hizi muwe tu mnatumiana PM huko...
 
Wimbo wenyewe nimesikiliza Mara moja Tu inatosha. Makelele mwanzo mwisho mashairi hakuna.
 
Wimbo wenyewe nimesikiliza Mara moja Tu inatosha. Makelele mwanzo mwisho mashairi hakuna.

Huu wimbo waliupania sana!wote wawili walikua na lengo la kufunikana mwishowe wameuharibu!!
Sauti zimebanwa sana kiasi cha kutosikika maneno!Melody mbaya kuliko
 
tatizo sio la bella tatizo aliekaribishwa ameimba kama kapanic au ana mashindano na mtu wimbo una makelele balaa, maji ukiyakamia sana hunywi.
 
Hii nyimbo nimeforce niipende ila imegoma kabisa.....barnaba na chamellione iko vyema kabisa
 
Back
Top Bottom