Christian Bella Ft Koffi Olomide

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,170
Reaction score
7,665
Leo Christian Bella Kaachia single ake alio mshirikisha Koffi Olomide Inayo itwa `ACHA KABISA' kama umepata wasaa wa kuisikiliza itakuwa pouwa

Sijaona wala kuelewa Alicho imba Koffi Olomide sijajua Kama ni ugeni wa Lugha anayo tumia Koffi Olomide au ni kweli hajawa katika Ubora wake.

Nimeona kafanya kazi bora kafanya Sio kama alivyo fanya kwenye nyimbo ake ile ya Ekotite! Hajafanya collabo kama kweli analengo la Kumuinua Christian Bella kimataifa zaidi! Na hii si nzuri kwa star kama Koffi kufanya Collabo kama kalazimishwa!

Kikubwa nilicho penda kwenye huu wimbo ni Vile Bella alivyo Imba kwa hisia kali! Vile Bella alivyo Lalamika naona Hapa Bella Kaimba vizuri zaidi Kuliko hata kwenye wimbo wake ule wa Amerudi na ule alioshirikishwa na Kiba

Kaandika historia ya kuimba na Olomide lakini Olomide hajataka historia yenye Ubora bali kataka Bora historia

Ni mtazamo wangu na wewe unaweza kuwa nao wako!
 
Mbona Koffi kaimba fresh tuu...
 
Nimeusikiliza zaidi ya mara kumi lakini sijauelewa kabisaaa
 
ekotite ekotitee ekotitee duh napenda hii ngoma mpaka naumwa hasa nikiwa na pesa yaan najikuta naimba tuuuu..
 
ekotite ekotitee ekotitee duh napenda hii ngoma mpaka naumwa hasa nikiwa na pesa yaan najikuta naimba tuuuu..

imekaaa kipedesheee! ekotitee ekotitee huku unahesabia kilundo cha ten ten ekotitee ekotitee
 
Labda hamjamuelewa Koffi. Ule ndio uimbaji wake hata kwenye nyimbo zake mwenyewe. Mara nyingi huwa anaweka watu wa kupandisha sauti Ili kuongeza vionjo. Koffi sio mtu wa kupiga mayowe anaimba sauti ya bass. Mnaosema Ana jealouse mmejuaje?
 
Kofii kaharbu bora bella angeimba peke yake

Kweli kofii kazengua sana ndo tabia ya wasanii wakubwa wanafanya collabo km wanalaZimishwa na hawataki nimekumbuka p.square walivyo muharibia wimbo A.y pia
 
Kwenye huu wimbo kuna vitu kadhaa vimenisikitisha sana.
1. Hii collabo ilikua imepangwa au ilitokea ghafla tu na muda ulikuwa limited so wakafanya bora iende?

2. Kwanin Bella hajaipa uzito ngoma hii ambayo karekod na mwanamuzik nguli na anaetamba kwa sasa Africa?

3. Kulikuwa na ulazima gani wa ngoma hyo kutolewa kwa pupa wakat bado #Nagharamia inahitaj booster?

4. Bella anajaribu kututhibitishia kuwa Nagharamia haikuwa kama ilivyotarajiwa? Hivyo anafanya ku-Compensate effect?

5. Bella hajaona kama wimbo uko chini ya kiwango ukilinganisha na uwezo wa waimbaji?

6. Kutoka ghafla tena bila mipango nAdhifu kuna uhusiano na show ya Koffie hapa bongo? (I.e Bella anatafuta namna ya kupanda jukwaaa moja na mzee mzima Olomide?)
Nawasilisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…