Christian Bella: Hakuna msanii asiyependa kufika alipofika Diamond Platnumz

Christian Bella: Hakuna msanii asiyependa kufika alipofika Diamond Platnumz

Kidingi

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2012
Posts
1,872
Reaction score
1,832
Christian Bella anaamini kuwa kikwazo cha wasanii wengi kukua kutokuwa na management. Bella ameiambia Bongo5 kuwa kila msanii ana lengo la kwenda mbali zaidi lakini tatizo lipo kwenye management.

"Muziki wetu bado una matatizo mengi ndo maana unaona kuna wakati unahitaji kufanya kitu lakini unashindwa. Hakuna msanii asiyependa kufika alipofika Diamond, kila mtu anataka, tatizo ni management," amesema msanii huyo.

"Kila msanii huwezi kutumia pesa yako ya mfukoni kutengeneza video, hautaweza kufika popote. Management ndIo inaweza kukusimaMia kila kitu, lakini sisi hapa kila kitu anafanya msanii huyo huyo, hatuwezi."


Chanzo: Bongo5
 
wanayempenda mwenyewe anamkubali Diamond lol...
 
Yap, tukiwa wakweli tutashinda, sio kukaa kudanganyana nimechelewesha video kisa xenophobia, zungumza ukweli tuu utaeleweka, mbona video za diamond anafanyia huko huko south na zazidi kutoka, management ni muhimu kwenye sanaa
 
Nimefurahi alichosema natumaini itasaidia kufungua wengine wakafanya mengi ili wapae pia.

Miziki mingine nasikiaga redioni nazipenda ila ndio usikii tena.

Inabidi nao wajitahidi kuambia hao nao wanataka kuona nini na nini kinafanyika inaelekea wanasikiliza tu.

Na pia uoga wa kuhama kwenda kwingine nahisi ni kikwazo ikitokea waliemuacha akaonga wasifanikiwe sababu hawali pesa zao tena.
 
Naomba mturushie basi link za miziki yake youtube etc tukaangalie
 
Watanzania tunapenda mafanikio lakini hatuwapendi waliofanikiwa! At least Bella Appreciates CC. Ruttashobolwa, Kimbley, PAULAkilaki, chige, mzurimie, rubii.
binti kiziwi, ahsante kwa taarifa kv hii sio habari manake kila mwenye ufahamu anauelewa huo ukweli! Ni mwanamuziki gani huyo Tanzania hii na hata nchi za jirani atakayekuwa na uthubutu wa kutotamani kufikia alipofikia Diamond... HAKUNA! Ni shabiki gani nchi hii ambae hatamani mtu anayemshabikia afikie japo nusu tu ya mafanikio ya kisanaa ya Diamond; HAKUNA... haya mengine ni blah blah tu!
 
ukweli utabaki ukweli na uwongo utajitenga...jitahidi anazofanya mond ndiyo mafanikio yanayoonekana now...wengi walijitahidi but mafanikio yalipoanza kuonekana wakalewa sifa....lkn kwa huyu dogo anazidi kukaza uzi....big up bella kwa kusema ukweli.
 
Back
Top Bottom