Christian Bwaya kuhusu mipango ya muda mrefu na muda mfupi ya wabunge

Christian Bwaya kuhusu mipango ya muda mrefu na muda mfupi ya wabunge

August

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2007
Posts
9,327
Reaction score
5,206
Akijibu hoja ya ukomo bungeni, Christian Bwaya ameandika:

"Wabunge wengi wana mipango ya muda mrefu kaka. Tuwaelewe.Miaka mitano ya mwanzo —kulipa madeni makubwa ya uchaguzi. Miaka mitano ya pili —kufanya uwekezaji mkubwa ili kuwa na nguvu ya kichumi.

Kuingia rasmi kwenye tabaka tukufu.Miaka mitano ya tatu —kutengeneza mtandao wa kudumu ikiwezekana ndoto kubwa zaidi za kisiasa zitimie.Miaka mitano ya nne —kujipanga namna ya kuwaelimisha wapiga kura kuwa jukumu la kujiletea maendeleo ni lao wenyewe.

Miaka mitano ya tano —kusisitiza falsafa ya kujitegemea ili wananchi waone haja ya kujiletea maendeleo yao wenyewe"


Lubasha Jr.png
"
 
Back
Top Bottom