Christian Dannemann Eriksen

Messi Lionel

Senior Member
Joined
Jan 11, 2018
Posts
170
Reaction score
159
(CHUMVI YA POCHETTINO)..

Achana na La Masia iliyomtoa Xaví,Iniesta na Fabragas,Achana Maanchester academy iliyomtoa fundi Paul Scholes..Achana na Bayern München academy iliyomtoa Bastian Schweinsteiger na Tony Kroos..

Siku chache zilizopita nilikuwa ma thread ya academy za soka zinazosadikika kuwa ni bora zaidi duniani...Ya kwanza ilikuwa Ni Ajax Amsterdam iliyoko.chini ya Ajax Amsterdam Fc..
Baada ya kutoka katika nchi ya maziwa na siagi Denmark..moja kati ya mataifa yanayojiweza Duniani Christian Alielekea katika Academy ya Ajax kupata uzoefu zaidi..
Ilikuwa ni katika miaka ya 2010..akiwa na umri wa miaka 18 tangu alipozaliwa Februari ya 1992..

kwa mara ya kwanza huyu fundi wa mpira nilimuona akiwa na Jezi ya Ajax akkwa dimbano mechi za Ligi ya mabingwa ulaya..uefa champs league..
Mwaka 2013 baada ya Christian kufanya makubwa akkwa Ajax..Maskauti wa Spurs walimuona Fundi wa mpira wakaishawishi Board ikambeba..
Niliwahi kuwaza maisha ya spurs bila ya Luca Modric na Gareth Bale...

Lakinj hili Jembe limefanya shughuli moja nzito sana kuhakikisha Spurs wanakuwa chama.la.ushindani sio ushiriki...Eriksen Anakaba..Anaichezesha timu mipira ya karibu na mbali..anapiga free kicks zote..Magoli ya mbali na ya muhimu..
Jamaa hata katika timu ya taifa jamaa ameibadilisha sana kiushindani..
Hana miaka miwili Eriksen ataanza kusumbuliwa na baruaa za kusajiliwa na Real Madrid na Bayern Munchen..

Spurs wamepita viungo mafundi wengi sana wa mpira kama Luca Modric, Tom Huddlestome,Scott Parker,Paulinho n.k

Lakink kwangu mimi bado nahisi watu wengi hawajafanikiwa kumuimba midomoni mwao..
Huyu kwangu ni Hero kweli kweli japo hazungumziwi sana kama Dele Ali,Harry Kane,Danny Rose.....

[HASHTAG]#footballaddicted[/HASHTAG]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…