Christiano Ronaldo atia aibu ya mwaka wakati wa kutambulishwa

uwe hodari

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2022
Posts
4,045
Reaction score
8,608
Hali ni mbaya mbaya sana kwa ndugu ronaldo hali iliyopelekea kutia aibu ya mwaka wakati akitambulishwa na klabu yake mpya huko bara asia

Alisikika akisema

"Kuja hapa South Africa sio mwisho wangu wa kucheza mpira".

Hali hii iliwaacha vinywa wazi mashabiki wake waliohudhuria wakati wa utambulisho wake.

Mashabiki walifura mitandaoni kwa matusi wakisema inawezekana vipi mchezaji anayelipwa paund milion 200 kwa mwaka hajui nchi anayoishi?

Ndugu yetu anaonekana mwili wake upo Asia ila akili zimebaki Europe.

Nashauri apunguziwe mshahara kwani hajaonyesha heshima kwa nchi.
 
Kukosea ni jambo la kawaida tu. Sijui umefanya tathmini ya wanamitandao wangapi ambao wanashutumu kuhusu jambo hilo lakini kubwa, club imetangaza kuwa na wafuasi wengi sana baada ya kutangaza kumsajili Cristian. Hili ni jambo jema kibiashara. Mengine, ni utashi wa kibinadam tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…