Elections 2010 Chuki dhidi ya CCM sio Magamba! Ni hawa wabunge wa CCM! Kumbuka Zitto- Buzwagi!!

Elections 2010 Chuki dhidi ya CCM sio Magamba! Ni hawa wabunge wa CCM! Kumbuka Zitto- Buzwagi!!

chidide

Member
Joined
Nov 11, 2010
Posts
91
Reaction score
9
Kwa mwenendo huu wa bunge naona ndio mwisho wa CCM.

Chanzo kikuu cha CCM kutofanya vizuri 2010 kinaanzia kwenye bunge la 2007 wakati wa hoja ya Zitto kuhusus mkataba wa Buzwagi kusainiwa London. Nina uhakika wengi wenu mlikuwa mnaangalia tukio lile bungeni kupitia TVs, mimi nakumbuka nilikaa mpaka saa saba na nilikuwa naumia sana roho kwa kulinganisha walichokua wanasema wabunge wa CCM na wa Upinzani. Tofauti ilikuwa kubwa sana na ukweli ulikuwa wazi sana. Matokeo yake Zitto aklfungiwa kuingia bungeni! Nakumbuka sura yake wakati anatoka bungeni usiku ule! Iliniumiza vibaya sana coz nilikuwa naona wazi kaonewa na wabunge wengi wa CCM wanatumia wingi wao kuzima hoja. Niliichukia CCM from then. Kesho yake dereva wangu alikuja kunichukua saa kumi na moja asubui. Baada ya salamu tuu alinieleza jinsi alivyochukizwa na wabunge wa CCM. Nae alikesha akingalia tukio lile. Nilipofika kazini, wafanyakazi wengi walikuwa wanaelezea tukio lile lile. Inaonyesha watu wengi (wa mijini waliokuwa wanaweza kuona tv) waliliangalia tukio lote lile. Hoja yangu hapa ni kuwa watu wengi tulichukizwa na unafiki wa wabunge wa CCM.

Nina hisi spika Sitta nae wakati suala lile linaelekea hatua ya kupiga kura kuwa Zitto kalidanganya bunge nae aliingiwa na hofu. Bado nakumbuka alivyowashauri wabunge wenzake kuwa makini sana na hatua wanayotaka kuchukua. Aliwaasa hivyo nadhani baada na yeye kuona uhalisia ulivyo. Lakini wabunge wa CCM hawakutaka kusikia la mtu. HAPO NDIPO HASIRA YA WANANCHI DHIDI YA CCM ILIPOAANZA! Maandamano ya kumpokea Zitto Dar es Salaam pale Ubungo mpaka Jangwani huku mvua kubwa ikinyesha wakati wote ndio kitu pekee kinachodhihirisha wananchi wamecho. Maana fikiria nani leo katika CCM anaweza kukusanya watu mia tuu akawahutubia huku mvua inanyesha? Labda awalipe kwanza!

Sitta na wenzanke walifanikiwa kiddogo kurudisha imani ya wannchi juu ya CCM walipoanzisha kilichoitwa vita dhidi ya ufisadi. Baadhi ya wannchi wakaona kumbe CCM bado ina watu wanaopinga ufisadi. Lakini hili limekua kumletea sitta matatizo ambayo kila mtu anayajua.

Sasa leo wabunge wanrudia kile kile kilichosababisha CCM ichukiwe, kupinga kila kinachosemwa na wapinzani, sisi wananchi tunaona na kusikia. Hasira dhidi ya CCM zinazidi kupanda. Kwa spika wa sasa naweza kusema hana uwezo wa kubadilisha upepo kama alivyofanya sitta wakati ule. Yeye nae atachukuliwa na upepo utakaoichukua CCM.
 
Back
Top Bottom