Chuki ya Watanzania dhidi ya watu hawa ilianzia wapi?

Sidhani kama ni kweli. Nchi zilizoendelea wafanyakazi incompetent hawajajaa sana na wangekuwa wamejaa sana basi ungekuta wako kama sisi. Kunaweza kuwa na elements ndogo ndogo lakini kwa ujumla ni wengi ni wachapakazi. Tanzania iko level nyingine na usijaribu kulinganisha na dunia nzima.
 
Afadhali umenisaidia kumuelimisha.
Halafu cha kuongezea wasomi wa nchi zingine wanajua wajibu wao huwa hawangoji hadi wawajibishwe au hadi sheria ichukue mkondo wake ndio ili waact.
Ni sawasawa na ule utamaduni wa waafrika kutupa takataka hovyo barabarani na mitaani eti kwa vile sheria haijamkataza kutupa wakati nchi za wenzetu kila raia anajua ni wajibu wake kuliweka jiji safi bila kuambiwa wala kushurutishwa.
 
Wenye nchi zao wanajua kuhusu incompetent workers
 
Kwa wale mnaodhani wazungu ni Mungu.
It's a global issue
 
Umewahi kusikia Broken window theory?
Siku ukienda kwenye nchi yenye mitaa misafi wewe mwenyewe hautatupa taka hovyo.
Mtu aliyezoea nchi safi akija nchi chafu baada ya muda na yeye ataanza kutupa taka kama wenyeji tu

Endelea kujidanganya kwamba nchi za nje ni safi bila sheria na usimamizi. Kuna kitu hamjui kuhusu binadamu. Unaona tuko tofauti lakini kiuhalisia tunafanana sana kuliko unavyodhania
 
Sawa tufanye kwetu ni pachafu kwa vile hakuna sheria,sasa unadhani ni kwa nini hizo sheria hazipo?
Maana yake viongozi wako hawajui vipaumbele au hawajui umuhimu wa hayo mambo ya usafi wanachukulie ni kitu cha kijinga so tunarudi palepale kuwa wasomi wetu wana matatizo.
 
Mtu anaposema wasomi ni wajinga na ndio chanzo cha Africa kutoendelea alipaswa aeleze pia ni kundi gani wanaloona linachangia maendeleo ya Africa mpaka waone wasomi ndio wanarudisha nyuma juhudi zao za kuiendeleza Africa

Walio kimbia shule Huko Ulaya ndo walioongoza kuleta innovations na kuajili wasomi.

Walio kimbia shule wa hapa Tanzania ndo wanaongoza kulaumu wasomi kwa kuto kuleta innovations kama waliwasomesha hivi.

Ni wapumbavu tu.
 
Viongozi ni asilimia ngapi ya wasomi. Siasa ni mchezo mchafu
Kwanza serikali ya Tanzania ukionekana tu ni mtu mwenye akili wanakunyamazisha chap
Wasomi wapo wengi wanaoweza kubadili taifa kwa kuanza kubadili mfumo wa hovyo na siasa chafu, lakini kwa Tanzania hawapewi nafasi, sasahivi wasomi wengi tu wenye uwezo wa uongozi wanaogopa kuingia siasa za Bongo
Na hii huwezi kulaumu wasomi wote, wakati hao viongozi hadi watu wasio wasomi wamechangia wao kuwepo hapo

Kila mzigo wa taifa mnawaangushia wasomi, kwa nini hamtaki watu wasio wasomi kuwa part ya tatizo? Bali kwenu tatizo ni wasomi sio?
 

Nakuongezea pia, Nchi zilizo endelea ni Raia wote wanajua na kutimiza wajibu wao ndo maana nchi inaendelea.

Ila huku Tz, Tunataka wasomi peke yao watimize wajibu wao kimiujiza, wakati kundi kubwa la wasio soma wapo wapo tu.
 
Wasiosoma huwa wanakata tamaa wanapoona waliosoma wanafanya mambo ya hovyo ndio maana hawa kidogo tunawapa excuse.
Maana ukimuuliza kwa nini umefanya hivi atakujibu kama Professor au Phd holder amefanya hivi mimi ni nani nisifanye?
Nakuongezea pia, Nchi zilizo endelea ni Raia wote wanajua na kutimiza wajibu wao ndo maana nchi inaendelea.

Ila huku Tz, Tunataka wasomi peke yao watimize wajibu wao kimiujiza, wakati kundi kubwa la wasio soma wapo wapo tu.
 
Aisee, you are out of touch. Mzee wa ku-google naona unautendea haki utanzania wako. Mtanzania tangu ajue kuna ku-google yeye mkibishana jambo dogo yeye ana-google na kuweka vitu ambavyo in context ni mbingu na ardhi. Wenzako tunazungumzia maisha tuliyoishi na kushuhudia kwa macho yetu.
 
Hizo documentary zinazoandikwa zinaongelea mambo ya wapi. Mars au?
 
Sidhani hata kiingereza kinapanda kwako. Huyo ni mtu mmoja analalamika, hawakilishi wote.
Bwana eeh haya mambo yako open mno, dunia nzima imejaa watu comprtent na incompetent
We endelea kuona wazungu ni binadamu perfect
 
Waajiriwa (police, walimu na wengineo wa serikalini ndio enzymes ya sisiemu- wanahongwa kidogo tu kwisha habari)
Wasomi- ndio wanaolirudisha taifa nyuma Kwa kipengele cha utendaji mbovu , maamuzi mabovu(mkataba) na uwizi uliopindukia na mengineyo yasiyoelezeka.
 
Huwa sielewi, chuki za Watanzania dhidi ya
1. Wasomi
2. Walimu
3. Waajiriwa

Ilianzia wapi. Kosa la hao watu ni nini maana nimeona threads nyingi zinaanzishwa kuwaponda.

They're just living their lives like everyone else. Why hating them?
Wanaochukiwa zaidi ni wale wenye pesa lakini hawana elimu wala shughuli yoyote rasmi(hustlers).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…