Chuki za kidini zinatoka wapi?

Chuki za kidini zinatoka wapi?

Peculiar

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2015
Posts
821
Reaction score
689
Wahenga wanasema,"hakuna mtu aliye mkamilifu"

Biblia inasema,'usihangaike na kibanzi kwenye jicho la mwenzio ilhali wewe una boriti kwenye jicho lako na huenda hujijui'

Qur'an inasema,"hakuna kulazimishana katika dini na mtu ambaye mnatofautiana Imani"

Imani zipo nyingi,Imani zipo nyingi lakini naomba nizizungumzie Imani hizi kuu mbili kwa hapa nchini kwetu na hata duniani kwa ujumla.

Hapa nitayazungumzia mambo ambayo kwa mtazamo wangu ndio yamekua yakitajwa sana katika mizozo ya kidini.ambayo kimsingi siioni sababu ya mizozo hiyo inayoleta chuki,maana katika hayo dini zote zinaongea lugha moja(zinaelewana) ila shida ni waamini.

Hizi dini hizi mbili MSINGI WAO MKUU NI KUAMINI KATIKA UWEPO NA UWEZO WA MUNGU. Dini hizi zina amini malaika,mitume na vitabu pia.

Japo kuwa kuna tofauti katika namna ya kuamini hivyo.lakini msingi unabaki kua ni kwamba "wanaamini"
Na hii ni kawaida,watu wanaweza kua na lengo moja lakini kila mtu akawa na njia/namna yake ya kulifikia lengo hilo.

Hizi dini mbili, zote ZINAHIMIZA UPENDO
Mfano: biblia inasema,'mpende jirani yako kama unavojipenda wewe' Qur'an inasema, mpende na mtendee wema jirani yako hata kama yeye si Imani moja na wewe'Kwa mfano huu unaona DINI KAMA DINI HAZINA MISINGI YA CHUKI KWA YULE ASIYEZIAMINI.

Dini hizi kwa sehemu kubwa zina Sheria zinazofanana. Mfano: Ziinakataza na kurusu mambo yote ila katika utaratibu wa dini husika.

MFANO SWALA LA KUUA
Qur'an inasema, atayeua mtu kwa makusudi naye auawe'. Biblia inasema,"atakayeua kwa upanga naye atauawa kwa upanga, sehemu nyingine inasema"mchawi hana haki ya kuishi"

Kuhusu mzinzi kuuawa. Biblia inasema ikiruhusu "asiye na dhambi tu ndio anayo haki ya kumrushia mawe mzizi hadi afe". Qur'an inasema,"akithibitika mzinifu aliyeeoa/kuolewa apigwe mawe na wale wanaojihisi wako safi(hawana dhambi) mpaka afe"

Ukija katika mavazi hizi dini zinafanana kama sio kabisa ni kwa sehemu kubwa. Biblia inasema,"mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanaume wala mwanaume asivae mavazi yampasayo mwanamke" Qur'an inasema,"ni haramu mwanaume kujifananisha na mwanamke kimavazi na urembo kama ilivyo haramu mwanamke kujifananisha na mwanaume.

✓ Kwa hiyo usihusishe uvaaji mbaya wa mtu na dini ya mtu.
Dini zote zinataka watu wavae vizuri na kujipamba na kujisitiri kulingana na jinsia zao.

Hakuna dini kati ya hizi mbili inaruhusu pombe wala nguruwe, kamari, ushirikina na mambo kamahayo.
Ukimuona mtu anakunywa pombe au anakula nguruwe.ni kwamba anafanya yeye kama yeye si kwamba anafanya kwa ruksa ya dini yake. Qur'an inasema,"mmeharamishiwa nyamafu na damu na nguruwe na mnyama aliyechinjwa kwa kunuia(jina) jina la asiye Mwenyezi mungu.

Biblia inasema," na huyo nguruwe kwa kuwa ni najisi kwenu,msile nyama yake wala msiguse mzoga wake"
✓dini zielewane lakini ,waamini hawa wasielewane katika kitu kile kile,tatizo linakua wapi?

Kuna hii hoja ya kupinga dini,((niipachikie kidogo kwa mtazamo wangu)
Dini zimeletwa, NI KWELI. Waliokuja walikua wa aina tofauti na malengo tofauti.wapo waliokuja kutawala(wakoloni),wapo waliokuja kufanya biashara,wapo waliokuja kueneza dini. Si Kila kinacholetwa ni kibaya, wakoloni na wafanyabiashara walikua wabaya kwetu, lakini wamisionari walikua na ubaya gani?

Ni sawa na mnaweza kuwa katika chombo cha usafiri au hata familia,lakini kila mmoja akawa na nia na malengo yake.

JE, NI SAWA KUWAHUKUMU WOTE KWA NIA NA MALENGO MMOJA WAO?
Familia moja hiyo hiyo inaweza toa mwalimu,ikatoa jambazi ikatoa daktari. Walioleta dini wasemwe kwa kuleta dini na waliokuja kufanya mengine wasemwe kwa hayo. Vingapi vizuri tunaletewa na ni vyakweli na vinatufaa kutoka kwa hao hao?

USHOGA, UGAIDI NA UKAFIRI. Hapa kumekua na kupakiana ubaya, kusingiziana, kukerana, KUDARAULIANA. Vitu ambavyo kwa hakika hakipo katika havipo kabisa katika hizi dini. KAFIRI ni mtu ambaye anampinga na hawamuamini mungu kabisa katika uwepo wake na uwezo wake.mfano wa mtu ambaye ni KAFIRI ni FARAO/FIRAUNI.na wanadini zote hizi wanazijua taarifa zake.

Je, unapomuita KAFIRI mtu anayemuamini mungu, anamuamini Ibrahimu kua ni baba wa imani sawa na wewe JE, HIYO NI DINI AU CHUKI?

UGAIDI ni (UUAJI). kuua mtu au watu wasio na hatia. Mfano wa UGAIDI ni amekuudhi kiongozi fulani,wewe unaenda kuua watu waliopo sokoni au ibadani. Unapomuita mtu GAIDI kwa sababu ya dini yake,mtu ambaye huna ushahidi amshawahi kuuwa hata mbu. JE, HIYO NI DINI AU CHUKI?

USHOGA NA USAGAJI. unapomuhusisha mtu na USHOGA au usagaji kwa sababu ya dini na dini yake inakataza hayo,JE,HIYO NI DINI AU CHUKI?

tabia mbaya mbaya za mtu binafsi kuzihusisha na dini ya mtu kwa sababu wewe si muumuni wa dini hiyo huko ndio Kukosa dini ya mungu na huo ndio USHETANI.
ni USHETANI kwa sababu sifa kuu ya shetani ni UHARIBIFU.

Hakuna shilingi yenye upande mmoja,huwezi KUAMINI uwepo wa MUNGU na usiamini uwepo wa shetani.
Shetani anajipenyeza kwenye nyumba za ibada,kwa viongozi wa kidini,serikali na taasisi.
Ndio maana wapo wanaouhubiri chuki dhidi ya dini nyingine wazi wazi na kwa siri.
Ndio mana biblia inasema,"sio wote wanaotaja mungu wataingia katika ufalme wake"
Qur'an inasema,'watakuja watu watafanya miujiza kwa jina la mungu lakini ni waongo.

Kwa hiyo ukijiona/ukijihisi unachuki dhidi ya dini isiyoyako,JUA ROHO YA SHETANI IMEJAA NDANI YA KIFUA CHAKO.

Ulishawahi kuona viongozi wakubwa wa kidini wakikejeliana/wakidharauliana/wakitukanana kwa sababu ya utofauti wa dini zao?
JE,wewe mwenye chuki za kidini unazijua dini kuliko wao?
Sasa kwa nini una CHUKI?

Wenye chuki za kidini wanashida gani?
Je,hawayaelewi vizuri mafundisho ya dini zao?
Au wanafundishwa hizi chuki?

Kwa mtazamo wangu,KUWA NA CHUKI SABABU YA DINI NI KUKOSA DINI MAANA HAKUNA DINI INAYOHUBIRI CHUKI.

na ikumbukwe hakuna mtakatifu na mkamilifu duniani,na mitume waliletwa kwa ajili hasa wale wadhambi kama Mimi na wewe.

Hivyo tusihukumiane maana MWISHO ni Bora kuliko mwanzo na kati.

Unayemuona leo mdhambi/kapotea huenda akabadilika na kua na mwisho mwema na mzuri kuliko wewe.

Qur'an inasema,"hakuna kulazimishana kutekeleza yaliyo katika dini ambayo mtu sio dini yake.

Mwisho dini zote zinasema mungu anasamehe.
Biblia inasema, "samehe nawe utasamehewa" pia inasema,"samehe saba mara sabini"
Qur'an inasema, mwenyezi Mungu ni msamehevu na anapenda kusamehe, sameheaneni "

Kwa hiyo una haja gani ya kumchukia mtu kwa sababu ya dini yake wakati hata kama yupo katika makosa MUNGU YUKO TAYARI KUMSAMEHE WAKATI WOWOTE?

Nimeandika haya sababu naona mitandaoni watu wanakoseana sana heshima,wanatetea dini zao kwa matusi na vitu kama hivyo,ambavyo kwa hakika havileti ustawi mwema.

Halafu haya mambo yapo mitandaoni zaidi,huku mitaani maisha ni fresh,
Wa dini hii anamuajiri wa dini ile.wa dini ile anamtibu wa dini hii,yani amani!

Sasa hii sumu mbaya ya kidini ya mitandaoni haipaswi kuingia mitaani,maana wanaoeneza chuki mitandaoni ndio hao hao tunaoishi nao mitaani.

CHUKI ZA KIDINI NI MBAYA,ACHA KUENEZA CHUKI,

TENDA HAKI, SAMBAZA UPENDO.
tuvumiliane!

Nb: andiko hili linawahusu wale wanaoamini uwepo wa MUNGU tu katika dini zao hizi mbili hasa.
 
Kwanza edit neno "mungu" iwe MUNGU au Mungu...Mzee hata kanunua za kiswahili huzijui?[emoji57][emoji57]Nitarudi
 
Dah fact mkuu lait tungekuwa na watu wenye kujielewa kama wewe kuhusu dini kusingekua na Mihemko ya ajabuajabu
 
Nani huyo analeta chuki za kidini Karne hii ya 21? Apigwe risasi

Lakin pia tusiwe tuna-confuse kati ya "fact" na "chuki" za kidini

Mfano mtu akisema:
"Football clubs kubwa Tanzania zinadhaminiwa na Waislamu"

Hapo ameonesha "chuki" au amesema "fact"?
Kama mazungumzo ni kuwa watu wa dini gani wanadhamini timu kubwa,ukisema kweli ilivyo utakua sahihi,na haileti ukakasi wowote.
Ila kama mazungumzo ni wadhamini wa timu kubwa,kataja dini zao inaleta ukakasi.
Kwa sababu sijawahi kusikia mdhamini wa timu akihusianisha udhamini wake na dini yake.
Wadhamini na wafadhili huhusianisha udhamini/ufadhili wao na majina yao/kampuni zao.

Na hawafanyi hivyo kwa sababu wanalenga kuunganisha watu na (kupata) kutoka kila upande bila kujali dini/rangi/kabila.
Kuingiza dini mahali kama hapo ni kutengeneza mpasuko katika jambo linalounganisha watu either kwa kujua au kutokujua.

Na kitu kibaya zaidi ambacho kinakuja kutafsirika kama ni chuki za kidini,ni pale watu wanapoingizia dini mahali isipohusika kwa hata kutumia uongo, matusi na uzishi kwa lengo la kuvuruga,kuchafua,kuudhiana na vitu kama hivyo.
Kitu ambacho hakileti afya kabisa katika jamii ya watu waliostaarabpika.

Ndio maana hata jk Nyerere aliheshimu sana dini na makabila ya watu,lakini alichukia na alipinga sana udini na ukabila.
Na ndio maana leo watu wanaishi mchanganyiko na dini zao na makabila yao kwa amani kabisa,wanaheshimiana na kuvumiliana.
Kwa hiyo haya yanayoendelea mitandaoni ni yakuyakataa kabisa maana hayana faida yoyote zaidi yaleta hisia za chuki,ubaguzi na utengano.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani huyo analeta chuki za kidini Karne hii ya 21? Apigwe risasi

Lakin pia tusiwe tuna-confuse kati ya "fact" na "chuki" za kidini

Mfano mtu akisema:
"Football clubs kubwa Tanzania zinadhaminiwa na Waislamu"

Hapo ameonesha "chuki" au amesema "fact"?
Kwanini usiseme tu zinadhaminiwa na Wahindi na waarabu koko?
 
Back
Top Bottom