kwa kweli mie picha hizi zinazoonesha watoto wa mitaani mara nyingi nikiziona hunifanya mnyonge hata siku nzima,na wkt mwingine ninalia maana hawa watoto wanapata sio shida tu ya kukosa chakula,elimu,tiba na sehemu salama za kuishi bali wana maisha ya hatari sana.kukosa kwao elimu na mambo wanayokumbana nayo huku wakiwa hawapati upendo anaostahili kupewa binadamu na hasa mtoto kutawafanya waje kuwa vijana wenye hasira,chuki na wasioogopa kufanya chochote hasa mabaya.hawa watoto leo ni malaika kama walivyo watoto wengine wote,lkn haya mazingira yatawafanya wawe viumbe wabaya sana.
SIO SIRI HUWA NAJIULIZAGA,HIVI MTU AKIWA KIONGOZI WA NCHI HUWA ANAONDOKWA NA ROHO YA HURUMA NA UBINADAMU?.
Kwa nini viongozi wa nchi yangu hawaumwi na roho kama jinsi inavyoniuma mie ninapowaona hawa watoto wa namna hii?
kama roho inawauma kwa nini hawafanyi kitu kumaliza hili tatizo?
kwa nini inawezekana kumjengea GAVANA wetu mjumba kama wa mbinguni badala ya kuprioritize vitu muhimu mojawapo ikiwa ni watoto wanaoteseka mitaani?
nina maswali mengi na kila ninapojiuliza hasira zangu zinazidi kupanda,nadhani napoteza muda kuuliza maswali ngoja nivue hichi kimini nitinge magwanda niingie msituni,nimechoka kulia kwa kuwaona ndugu zangu wakiteseka.
i will be back.