bryan2
JF-Expert Member
- Jun 8, 2016
- 3,323
- 4,679
Wapendwa afya ni mtaji kwa kila kitu ukitaka kufahamu hilo umwa hata mafua tu ndio utajua afya ikipata shida kidogo tu hakika mwili ndio unaumia na hatimaye kudhoofu na kuchoka kabisa na mhusika kukosa furaha/amani.
Ukitaka kujua afya ni mtaji angalia ule msafara kwa kwenda kwa Babu Loliondo-Samunge hakika kila mtu alitaka kupiga kikombe either kupata nafuu au kupona kabisa maradhi yaliyokua yanamsumbua.
Kichwa cha mada kinahusika, sasa ulaji mbovu pamoja na madhara yake pasipo na shaka linaenda kuwa tatizo la kitaifa soon.
Siku hizi watu haumwi sana malaria au kifua kikuu magonjwa yatokanayo na ulaji mbovu yanakuja kwa kasi. Na baadhi ya magonjwa hayo ni kama vile;
- Sukari ya Juu/diabetes Mellitus
- Shinikizo la juu la damu/hypertension
- Uzito mkubwa/overweight
- Gout
- Magonjwa ya mifupa/rheumatoid athritis nk.
Magonjwa hayo na mengineyo hakika yamekua changamoto kuna asilimia kubwa sana kuongezeka kwa magonjwa hayo sio vijana wala wazee. Ukiangalia kliniki ya maradhi hayo watu wanavyojaa ndio utajua kuna shida zaidi.
Ubaya watu wanakula hovyo halafu hakuna mazoezi mtu anakula chapati na supu asubuhi then anakaa ofisini mchana anakula chips then ofisini akirudi nyumbani ugali mkubwa then kulala hakuna mazoezi zaidi maradhi hayo bado kuna kuvimbiwa tena maudhi madogo madogo.
Bila kusahau vidonda vya tumbo/pud, mafuta kuwa juu/cholestrol/hyperlipidaemia, bado ni matokeo ya ulaji mbovu.
Hili ni suala mtambuka kuanzia kwenye jamii hadi taifa, watu waelekezwe ulaji bora, kuna wataalamu wa lishe kila wilaya wafundishe watu.
Kuwe na siku ya kitaifa ya kufanya mazoezi, litiliwe mkazo hasa watumishi wa ofisi za umma na binafsi, pia kwa mtu binafsi jipangie ratiba ya kupiga matizi.
Tuepuke vyakula hatarishi kwa afya zetu na pia tuwe na tabia za kupima afya zetu tusingoje tuwe hoi ndio tukimbilie hospitali.
Chagua afya bora kwa maendeleo yako na taifa.