Chukua Tahadhari unapopishana na Magari yanayobeba kemikali za sumu ikiwemo ya Sianidi inayotumika kuchenjulia dhahabu

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Wananchi na watumiaji wa vyombo vya moto wamehimizwa kuwa makini wanapoyapita magari hayo ili kuepuka kuyagonga. Pia wametakiwa kutolisogelea gari lililobeba kemikali ya sianidi (Sodium Cyanide) pindi linapopata ajali badala yake wachukue tahadhari kwa kukaa umbali wa mita 100 ili kutopata madhara mbalimbali ikiwemo ya kupoteza maisha pindi wakivuta hewa yenye sumu inayotokana na kemikali hiyo.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkemia kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Derick Masako wakati wa uzinduzi wa kampeni ya utoaji wa elimu kwa Umma hasa watu wanaoishi pembezoni mwa barabara iliyofanyika katika kituo cha daladala Mbezi Luis.

Kampeni hiyo inaendeshwa na kampuni ya usafirishaji wa kemikali ya Taifa Transport and Logistic Limited, Kampuni ya Freight Forwarders Tanzania, Mainline Carriers pamoja na Swala Solution Limited.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo, Masako amesema kemikali hiyo ya Sianidi imeanza kuingia nchini tangu mwaka 1990 na toka wakati huo hadi leo imekuwa ikisafirishwa bila kuleta madhara yoyote kwa binadamu.

“Ajali za kemikali hii ziliwahi kutokea mbili moja gari lilipinduka katika mkoa wa Singida na nyingine kontena lilianguka mkoa wa Shinyanga, lakini kutokana na kwamba wale wasafirishaji walikuwa na elimu waliweza kuwazuia wananchi wasisogee eneo la tukio. Kemikali hii ikimwagika na kuchanganyika na maji inaweza kuleta madhara makubwa kwa binadamu kwani inatoa hewa chafu ya sumu ambayo mtu akiivuta inaweza kumsababishia kifo kwa haraka,” amesema Masako
WhatsApp-Image-2024-11-04-at-17.23.56_b7db4adf.jpg

Baadhi ya Magari yaliyobeba Kemikali ya Sianidi ambayo Msafara wake unakuwa ni Magari 12 ambapo yenye Kemikali yanakuwa ni Malori 10 (yenye namba 1-10) huku yakiongozwa na Magari madogo Mawili moja mbele ya msafara na lingine nyuma ya Msafara ili kutoa Ishara.

Amesisitiza kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali anasimamia sheria tatu ambazo ni usimamizi wa kemikali za viwandani na majumbani, sheria ya usimamizi wa taarifa za vinasaba za binadamu na mwisho ni ile inayohusu mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali.

“Mbali ya sheria hizo Mkemia Mkuu wa Serikali anasimamia kituo cha udhibiti wa matukio ya sumu. hivyo mamlaka inajukumu la kuwasisitizia wadau wanaosafirisha kemikali hizi kuendelea kutoa elimu kwa jamii, hata hivyo Kemikali hii ya sianidi ndiyo inayotoa dhahabu kwenye miamba,” amesema

Naye Ofisa Usalama Mahala pa Kazi kampuni ya Taifa Transport and Logistic Limited, Bestina Kitinya amesema hatua ya kwanza ya kujikinga na kemikali hiyo pindi ikimwagika barabarani basi watu watakaokuwepo eneo hilo watapaswa kuvaa barakoa na kukimbia umbali wa mita 100.

“Na unapokimbia hakikisha unakimbia kwa kuangalia upepo unapotokea, pia ikitokea mtu amemgusa yule ambaye ameathirika na kemikali hiyo ya Sianidi mfano dereva aliyekuwa akiendesha gari bila kujikinga anaweza kupata madhara pia, hivyo unapaswa kutomgusa sehemu zenye jasho,” amesema

Naye Mratibu wa Usalama, Afya na Mazingira kutoka Kampuni ya usafirishaji ya Freight Forwarders Tanzania, Sadiki Yusufu amesema elimu hiyo ni muhimu kwa jamii kwani kemikali hiyo ni muhimu katika sekta ya uchimbaji dhahabu duniani kwani ina uwezo mkubwa wa kuondoa dhahabu kwenye mwamba.
 
kwani ina madhara gani? kwanini wasiibebe kwa treni?
 
View attachment 3143486

Wanayoyaongoza hayo magari wanatakiwa wayalinde ili msafara usiingiliane na magari mwengine.
 
Hatari sana, wangetafuta namna nyingine yakusafirisha hiyo sumu baadala ya Barabara, maeneo ya migodi ni kanda ya ziwa.

Pale Isaka kuna reli, kuwe na special wagons zenye strong layers Kwa nje na kontena inawekwa ndani, wanashusha Isaka au Mwanza the malori yanachukua hapo kuelekea huko migodini under special escort.
 
Serikali isiishie tu kwenye usafirishaji wa sumu.

Kuna changamoto kanda ya ziwa ya wachimbaji wadowadogo kutumia chemicals kama mercury, cyanide nk kwenye kazi za uchimbaji na uchenjuaji wa dhahabu.
Plants zimezagaa kila mahala, mialo ya uchenjuaji kila mahala na hii kazi inatumia maji yanayotiririshwa kwenye vyanzo mitaani na kwenye makazi ya watu na mwisho maji yote yanakwenda kuishiwa ziwani.

Nina wasiwasi sana na usimamizi wa hizi chemicals kwa wachimbaji wadogowadogo na hatari ya Afya za watu.
 
Back
Top Bottom