Dr Luu
JF-Expert Member
- Nov 24, 2016
- 489
- 386
Habari, kama kichwa cha habari kinavyo nielezea hapo juu. Mimi ninauzoefu kwa kiasi juu ya vyakula kwa kuwa ni mtafiti, tabibu na ninamiliki duka la rejareja ingawa sipati muda wakuka mara nyingi dukani ila naona brands nyingi zikiingia sokoni tena tunazipata kwa bei nafuu, kutokana na wateja wengi kuhitaji bidha za bei nafuu na ushindani wa kibiashara tulilazimika kununua bidhaa hizo. Dukani tuna mafuta ya alizeti, safi na brand nyingine zinazo badilika badilika ila hizi brand nyingine ndio zinanunuliwa zaidi kutokana na bei kuwa nafuu zaidi.
Nimekua nikipata wagonjwa wa ngozi wengi na wengi wamekua wakipata matatizo ya ngozi maeneo ya usoni, mapajani na katikati ya vidole vya mikono kutoka vipele vyenye kutoa majimaji au usaha na muwasho wa mwili au sehemu yenye vipele. Hili likanipelekea kumwambia kijana wa dukani kwangu afanye utafiti wa kuwauliza baadhi ya wateja (waliozoeana) watumiaji wa mafuta hayo ya bei nafuu juu ya afya zao hasa ngozi. Na mimi sikusita kubadili mafuta ya nyumbani kwangu kwakuwa tulikua tunatumia alizeti basi tukabadili na kuanza kutumia hayo ya bei nafuu.
Matokeo yalitustusha ndani ya siku tatu tu watoto wakanza kutokwa na vipele mikononi hasa eneo la viganja kwenye ngozi laini na katikati ya vidole. Hii ikanishtusha na feedback ya wateja pia zaidi ya asilimia 40% walikua na matatizo hayo hii ikalazimika kuachana na hizo bidhaa ingawa Kuna baadhi ya wateja wanayaulizia Kila kukicha hivyo tumekua tukiwaabarisha juu ya madhara ingawa wengi hawajali.
Hii imenibidi kuchukua hatuna na kuandika Uzi huu ili kuwaabarisha juu ya hili tulichukulie uangalifu, na wito kwa serikali na mamlaka husika juu ya hili.
TAHADHARI na pole kwa walao kwa mamantilie.
Asante!