IsangulaKG
JF-Expert Member
- Oct 14, 2010
- 706
- 386
CHUNGU KIFUKAPO MOSHI, VIPIKWAVYO VYAUNGUA
Ninaleta fikirishi, watunzi kulitengua
Zimezidi kashikashi, si zile nilichagua
Uzombi ninaoishi, kifuani naugua
Chungu kifukapo Moshi, Vipikwavyo vyaungua
Chungu Moshi kifukapo, vyaungulia vipikwa
Leo nikipiga Kopo, kesho rumande naswekwa
Yanilemea mikopo, ufukara nimevikwa

Zina misumali Ndala, nizidishe kuzivaa
Japo sina pa kulala, mapema nitoke baa
Kichelewapo Chakula, nisiseme nina njaa

Japo naumwa sauti, nizidishe mapambio
Kila nikivaa koti, lifunike masikio
Zikinitoroka noti, nicheke paso kilio

Nitazamapo kioo, bongebonge nimuone
Ingawa sipati choo, niseme mimi mnene
Tena nikikabwa koo, tabasamu lijazane

Nitishiwapo risasi, nijivike kunyamaa
Nihisipo ni kisasi, niseme ni ujamaa
Na amsemaye Bosi, nimuone ni kichaa

Tafsiri ya amani, iwe kujifanya bubu
Vyeti vyangu kabatini,visinipe majawabu
Uchumi ukiwa chini, niwalaumu mababu

Kifukapo Moshi Chungu, vipikwa vyaungulia
Alichochagua Mungu, si haki kukililia
Yakinizidi machungu, nje naweza kimbilia

malenga wa Ngumbalu
Grupo público Kisima Cha Mashairi | Facebook