SoC01 Chungu na Tamu Tozo za Miamala ya Simu

Stories of Change - 2021 Competition

Kaunga Maulid

New Member
Joined
Jul 13, 2021
Posts
4
Reaction score
0
Tanzania ni taifa lenye watu wa hali mbali mbali, wengi wao wakiwa ni wavuja jasho, walala hoi, kula kwao ni kwa mahangaiko, wanachokipata kwa siku huishia mdomoni mwao huku walio juu hawakumbuki hisani ya wanaowazunguuka na wakiziba masikio yao kunenepesha matumbo yao na familiya zao tu.

Watu wake wamekuwa wakifarijiwa kwa kauli mbalimbali ili kupambana katika kuondokana na hali hiyo ya umasikini inayowatafuna watanzania masikini mara utasikia “Kilimo ni uti wa mgongo kwa watanzania” lakini uwezeshwaji wa pembejeo hakuna kabisa.

Siku zote hakuna wanachokipata hata kile kidogo wanachopigania wananyang’anywa kila siku jua lao, mvua yao na hakuna anaewaonea huruma maana imefikia hatua sasa watanzania wakiimba wimbo mmoja sio mchana wala usiku utasikia “ukiweka unakatwa ukitoa unakatwa maisha yetu ni kibubu,” yaani makali kote kote daaah inauma sana.

Tulipotoka

Mambo yalianza kama mzaha tu kutoka kinywani kwa Mhe. Mussa Hazani Zungu ambae ni mbunge katika manispaa ya ilala kwa sasa ikiwa ni jiji jipya la mji wa Dar Es salaam.

Sauti yenye mamlaka kutoka kwa mbunge asiyekuwa na majivuno, mwingi wa fikra pevu na mchache wa majigambo yasiyokuwa na manufaa ndani ya jiji lake, ilipasua anga kutoka katika halmashauri hadi bungeni na kukamata hisia za wabunge na kuupitisha kuwa ni sharia sasa.

Hakika lisemwalo lipo na kama halipo basi linakula, hizi ni moja ya kauli za wahenga ambazo zimekuwa na tafsiri kubwa na zenye maana halisi katika maisha tunayoishi kwa sasa si masikini wala tajiri wote tupo katika mfuko wa mshikamano ili kuijenga Tanzania yetu.

Machozi ya damu na vilio vya wananchi kila kona ya Tanzania hakuna anaesikia sauti hizo za wavuja jasho, huku wakipigilia msumari kwa wananchi kuwa na ada ya ziada katika tozo za miamala ya simu kwani kulipa kodi ni uzalendo.

Wakati vilio vya wananchi vikiendelea kutokana na kauli ya waziri wa fedha na mipango Mh Mwigulu Nchemba ya hivi karibuni ya kupanda kwa tozo za miamala wataalamu mbalimbali wamekuwa na mtazamo tofauti tofauti kutokana na tozo hizi za miamala.

Prof. Wiketye asema tozo zitasaidia Uchumi

Mtaalamu wa masuala ya uchumi kutoka chuo kikuu cha Iringa Prof. Enock Wiketye ambaye ameelezea namna ambavyo tozo hizi zitakavyosaidia uchumi wa ta taifa letu la Tanzania na wananchi kwa ujumla.

Pro. Wiketye anawatoa wasiwasi watanzania kwa kusema kuwa tozo hizi za miamala ya simu ni aina ya kodi kama zilivyo kodi zingine hivyo wananchi wajivunie kulipa ili tuiendeleze nchi yetu kwa pamoja kwa kushikamana kama ilivyo tambulishwa kodi hii ni ya mfuko wa mshikamano.

Tathimini ya Profesa huyu ni kuwatoa wananchi gizani wenye mtazamo hasi kutaka kukwepa kulipa kodi ya mshikamano ambayo ina faida nyingi katika taifa letu na kwa manufaa ya wananchi wenyewe kwani maendeleo yote ya nchi hujengwa kwa kodi za wananchi wenyewe.

Ukweli wa jambo hili ni kuwa, kodi hii ni kwa ajili ya kuendeleza miradi mbalimbali ya serikali kwa sababu kuna huduma kama vile ujenzi wa barabara na elimu hakuna sekta nyingine inayoweza kuzifanya zaidi ya serikali.

Utamu wa madini haya ya Profesa Wiketye kutoka katika moja ya chuo bora nchini Tanzania yanatufanya kuiona Tanzania ijayo yenye neema tele kwani mtu ambaye analipa tozo hawezi kuiona faida mwanzoni mpaka itakapokuja kuleta matokeo mfano ujenzi wa barabara za vijijini utasaidia uchukuzi wa bidhaa kwahiyo mtu hawezi kuona hilo mwanzoni.

Maumivu ya Tozo

Tozo hizi imeonekana inawaumiza zaidi wafanya biashara kuliko ambavyo serikali itafaidika na tozo hizo lakini haiwezi badilisha msimamo wa raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan mwenye fikra pevu katika kuivusha Tanzania yetu mpya.

Lakini pia profesa anawatonesha vidonda na kuwaacha vikivilia damu kwa kusema kuwa serikali haiwezi kuitoa hii tozo lakini imesikia vilio vya wananchi wengi hivyo imepanga kuja na mkakati mwingine wa kutafuta chanzo kingine cha mapato ili kupunguza gharama za tozo ili kuwafanya wananchi wengi kuweza kumudu gharama hizo.

Wako tayari kufunga vitabu vyao, kufunga vibanda vyao na wengine wako tayari kugeuza vibanda vyao kuwa kuni ili kuchomea vitumbua maana hakuna wanachokifanya Zaidi ya kuingia hasara ya kununua bando na kusikiliza Waziri kaongea nini kuhusu miamala.

Ukweli siwezi kufuta mapendekezo maana bunge lishapitisha na imesainiwa na raisi tayari, hivyo ishakuwa ni sharia na kama anaeona hawezi kulipa hii kodi basi ahamie Burundi, ni kauli iliyochoma mioyo ya watanzania masikini daaaah inauma sana kwa kweli mtaji ni wangu, kibanda ni change, maamuzi ya kufanya biashara hii ni yangu mwenyewe lakini bado naonewa kiasi hiki? bora nikauze maji barabarani.

Mawakala wamekimbia vibanda vyao kwani upandaji huo unawaumiza sana wananchi wa hali ya chini ambao wanatoa na kuweka kiasi kidogo cha fedha kwenye simu zao, na kwa kiasi fulani baadi ya wateja wamepungua na kukimbilia benki hasa wale ambao wanatoa au kuweka kiasi kikubwa cha fedha.

Swali kubwa ambalo wakala wamekuwa wakijiuliza: Faida itaendelea ile ile tuliyokuwa tukipata hapo awali au tuendelee kuchapa kazi kwasababu wananchi wenye kipato kidogo ndio wanaolalamikia sana tozo hizi mpya ambao ndio wateja wakubwa kwa sasa na hawawezi kukimbia huduma hii kutokana na uwezo mdogo waliokua nao.

Serikali haiwajali kwa chochote mawakala katika tozo hizi japo wamekuwa wakiwaongezea faida wao tu serikalini.

Ikiwa wateja wengi wamekimbilia benki, hakuna wanachopata, kazi yao imekuwa ni kucheza bao na kushinda kiweni wakibishana kuhusu mpira na zisipopunguzwa tozo hizi wengi wao watakosa kabisa wateja na biashara nyingi zitakufa.

Hakuna anaepata faida iwe biashara ya mtandaoni au dukani ukitumia tu miamala kwenye malipo lazima ukumbane na changamoto hii ukitoa unakatwa ukiweka unakatwa yaani moto juu ya moto mpaka kieleweke.

Imefikia muda sasa watu hawataki kutuma hela kwa sababu ya tozo kwani gharama zimekuwa juu sana hakika cha kale ni dhahabu si ajizi kuona biashara ya vibubu na kutuma pesa kwa kutumia bahasha kwenye magari kushika hatamu kipindi hiki.

Kilio cha Wananchi

Vilio na malalamiko makubwa ya wananchi wizara ya fedha na mipango imepokea kwa mikono miwili maelekezo kutoka ofisi ya rais ili kuona ni kipi kimfaacho mtu katika tozo hizo.

Ikiwa taarifa iliyotolewa na waziri mwenye dhamana ya fedha ambapo wizara yake itafanya baadhi ya marekebisho juu ya tozo hizo kwa wananchi wazalendo walipa kodi.

Lakini hii haimaanishi kuwa marekebisho hayo yatafuta tozo hiyo ila yanatabiriwa kuleta afueni kwa watumiaji wa huduma za kifedha kupitia mitandao mbalimbali ya simu njia ambayo imekua ikitumika sana hivi karibuni.

Shauku ya watanzania ni kuona hata wao wanaotunga na kupitisha hizi sharia basi wahusike kwa namna moja ama nyingine kwani sheria ni msumeno unakata kote kote, wao pia ni watanzania na kulipa kodi ni uzalendo halisi na kwa maendeleo ya taofa letu sote.
 
Upvote 0

Back
Top Bottom