ndyoko
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,971
- 1,652
Ni mkasa wa fundu ujenzi na msaidizi wake ulotokea juzi
morogoro mjini kasoro bahari. Umalaya mwingine wa
kijinga kweli. Huku akijua kula na kuvaa kwake kunamtegemea
fundi wake, akaona haitoshi. Msaidizi wa fundi akaamua
kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa fundi wake.
Fundi alipojua, wala hakuwa na papara. Wakati wakiwa kwenye
kazi zao za ujenzi, alipopewa tofali (la siment) akalipokea
kisha akamwambia msaidizi wake ampe mchanga wa kujengea.
Ile msaidizi anainama kuweka mchanga kwenye kalai,
yule fundi akamdondoshea kichwani tofali toka juu
alikokuwa amelishikilia.
Hadi sasa jamaa amelazwa hospitali ya mkoa fahamu bado
hazijamrudia. Wanaowajua wanadai huyo fundi kafanya
makusudi ili amtoe roho mwenzake maana alishawahi
kusema kwa watu wengine kuwa aliapa lazima aje amfanyie
kitu mbaya huyo mwizi wa mkewe.
My take: Jamani wanaume tuache ukware wa kijinga, wanawake
wote waliojaa mitaani, mtu unaona haitoshi hadi, iweje
'utembee' na mke wa mtu ambaye ndiye anayekusaidia
kupata 'mkate' wako wa kila siku, mweeeeeee!