Chungu ya mke wa mtu: Yalomkuta mwenzetu huzuni tupu!

ndyoko

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
4,971
Reaction score
1,652
Ni mkasa wa fundu ujenzi na msaidizi wake ulotokea juzi
morogoro mjini kasoro bahari. Umalaya mwingine wa
kijinga kweli. Huku akijua kula na kuvaa kwake kunamtegemea
fundi wake, akaona haitoshi. Msaidizi wa fundi akaamua
kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa fundi wake.

Fundi alipojua, wala hakuwa na papara. Wakati wakiwa kwenye
kazi zao za ujenzi, alipopewa tofali (la siment) akalipokea
kisha akamwambia msaidizi wake ampe mchanga wa kujengea.
Ile msaidizi anainama kuweka mchanga kwenye kalai,
yule fundi akamdondoshea kichwani tofali toka juu
alikokuwa amelishikilia.

Hadi sasa jamaa amelazwa hospitali ya mkoa fahamu bado
hazijamrudia. Wanaowajua wanadai huyo fundi kafanya
makusudi ili amtoe roho mwenzake maana alishawahi
kusema kwa watu wengine kuwa aliapa lazima aje amfanyie
kitu mbaya huyo mwizi wa mkewe.

My take: Jamani wanaume tuache ukware wa kijinga, wanawake
wote waliojaa mitaani, mtu unaona haitoshi hadi, iweje
'utembee' na mke wa mtu ambaye ndiye anayekusaidia
kupata 'mkate' wako wa kila siku, mweeeeeee!
 
Sasa kamfanyia ubaya jamaa na mke wake wala hajamgusa?
 
Kuua ni jambo baya, ila kwa namna yeyote ile siwezi kutetea vitendo vya uhuni wa namna hii hata kidogo ...
Angemponda nalo sehemu nyingine ili iwe ni fundisho kwa wote wenye tabia kama hizi ....
 
Mke aliposikia habari hiyo bila shaka alichanganya na zake...na kiutu uzima alijipima mwenyewe!

Baada ya kusikia issue ilomkuta 'mpenziwe', nduguze walimwambia aondoke kwanza. inasemekana amaeenda kwao mang'ula, kilombero kwa muda.
 
hilo ndilo wanalo litafuta wala wake za watu..
 
Mie nilifikiri alimkamata 'live' na kumfanyia kitu mbaya napohapo. Alivyofanya huyo fundi mkuu ni mauaji ya kukusudia. Sheria itambana sana, na hatoweza kutaja kwamba marehemu alikuwa na tabia ya kumega mke wake.
 
Hapo penye red, alijuaje au ni hisia! Was there proof beyond reasonable dout? Sio kwamba nashabikia hilo, hapana ila kuhisi ukamuua mwenzako !! kwa ushahidi gani usio kuwa na mashaka? Kesho mtu akikuhisi anakuua bila ushahidi. If it were me I will sue him of tort of neglegence and surely I will succeed!!
 
Faida gani kapata kama akifa huyo mwanaume.

Sioniu zaidi ya kuzidisha kubeba dhambi ambazo haziwezekani kukwepwa, na kujitesa ye mwenyewe dunaini na adhabu za dunia, na moja wapo jela inamgoja :cool2:
 
Hajamgusa kwa maana ya hata kibao hajamchapa.....au nyumbani pamechimbika?

watu walihisi huenda ndo kaamua kumalizana na mgoni wake then aangemrudi mkewe. Hakuwahi kumgusa aliwahi kuondoka. ila kuna uwezekanao naye angemalizana naye maana alikuwa kama kapagawa vile!
 
Alilofanya linaweza kuwa kosa kubwa sana kwake
Duh kumdondoshea mwenzake tofali ni balaa
 
Faida gani kapata kama akifa huyo mwanaume.

Sioniu zaidi ya kuzidisha kubeba dhambi ambazo haziwezekani kukwepwa, na kujitesa ye mwenyewe dunaini na adhabu za dunia, na moja wapo jela inamgoja :cool2:

Kwani mtu anapata faida gani anpotenda dhambi ya kutembea na mke wa mtu?
 
nikuulize swali mkuu. Hivi ukimkuta keo analiwa denda au unamuona anatoka chumbani, say, guest na mwanaume unaweza ukasema hapo ametoka kusex au laah? maana huna uhakika kama kweli wamesex au laaah. unless uwakute wameng'ang'aniana ndo unaweza uka-prove beyond pasipo shaka. Kuna ushahidi wa mazingira au hata huo huuamini.
 
Mie nilifikiri alimkamata 'live' na kumfanyia kitu mbaya napohapo. Alivyofanya huyo fundi mkuu ni mauaji ya kukusudia. Sheria itambana sana, na hatoweza kutaja kwamba marehemu alikuwa na tabia ya kumega mke wake.

ni kweli yeye aichotaka ni kumtoa duniani sema alishindwa
 
Kwani mtu anapata faida gani anpotenda dhambi ya kutembea na mke wa mtu?
Kosa la nani mwanaume au mwanamke?

Sidhani kama mwanamke ana msimamo wa kuheshimu ndoa yake anagawa K nje.

Kama mke wako anagawa K nje basi huyo sio wakusihi naye, wacha ajiendee kwao salama salimini, na wewe uishi salama salimini.

Wavumilivu hula mbivu haita pita siku utapata mke wa maana.
 
Faida gani kapata kama akifa huyo mwanaume.

Sioniu zaidi ya kuzidisha kubeba dhambi ambazo haziwezekani kukwepwa, na kujitesa ye mwenyewe dunaini na adhabu za dunia, na moja wapo jela inamgoja :cool2:

Kuna watu wengine hata hawajali kabisa, anaona bora jela kuliko akuache hivi hivi!!!
 
Mie nilifikiri alimkamata 'live' na kumfanyia kitu mbaya napohapo. Alivyofanya huyo fundi mkuu ni mauaji ya kukusudia. Sheria itambana sana, na hatoweza kutaja kwamba marehemu alikuwa na tabia ya kumega mke wake.
.........na mahakamani kwenye kesi ya mada hawezi ku plead 'temporary insanity',huyu ni kitanzi tu.
 
Personally huwa nashangaaga mbona kuna mafree lance kibao mtaani inakuwaje unakula kichwa na mwenzio.
Ingefaa afe tuu bse huwezi kumega mke wa mwenzio and go unpunished
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…