Chunguza video hizi zinazotoa taswira za biashara ya madawa ya kulevya

Chunguza video hizi zinazotoa taswira za biashara ya madawa ya kulevya

kabindi

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
333
Reaction score
120
Fungua video hizi kupitia youtube uone ugumu wa kupambana na biashara ya amadawa ya kulevya. Utajifunza mengi ni jinsi gani Serikali zetu zinavyopata kigugumizi katika kudhibiti biashara hii.


Jicho Pevu Paruwanja la Mihadarati Part 1 - YouTube
Jicho Pevu Pawanja la Mihadarati Part 2 - YouTube
Jicho Pevu: Parawanja la Mihadarati Part 3 & 4 - YouTube

Ni kama cinema lakini ni ukweli ambao unathibitishwa na waandishi wa habari makini sana kupata kutokea kutoka KTN. Ukishindwa kufungua, copy title hizi moja baada ya nyingine na search kwenye youtube, tulia angalia harafu linganisha na kinachoendelea Tanzania.

[h=1]1. Jicho Pevu Paruwanja la Mihadarati Part 1,[/h] [h=1]2. Jicho Pevu Pawanja la Mihadarati Part 2[/h] [h=1]3. Jicho Pevu: Parawanja la Mihadarati Part 3 & 4[/h]
 
Ntarudi asubuhi, saa hivi nitalitikisa pilau langu na biya bure.
 
Ntarudi asubuhi, saa hivi nitalitikisa pilau langu na biya bure.

Mr.Kongosho malizia pilau lako na rudi asubuhi uangalie video hizi uone ni jinsi gani kulivyo na ugumu wa kupambana na biashara ya madawa ya kulevya. Lakini pia uangalie ni jinsi gani fascinating journalists wanavyoweza kufanya coverage ya taarifa muhimu na za siri kwenda kwa jamii. Hapa Kenya ni mfano tu lakini inawezekana hiki ndicho kinachoendelea kwa serikali nyingi duniani na pengine kwa kushirikiana na baadhi ya taasisi za dini, vikundi vya kiharamia na mengineyo mengi.
 
.....

Ni kama cinema lakini ni ukweli ambao unathibitishwa na waandishi wa habari makini sana kupata kutokea kutoka KTN. Ukishindwa kufungua, copy title hizi moja baada ya nyingine na search kwenye youtube, tulia angalia harafu linganisha na kinachoendelea Tanzania.

....

Mohamed Ali wa KTN(JICHO PEVU) ...ni kiboko...kwa kweli amelitendea haki jina lake( rejea Mohamed Ali Bondia wa USA).

Nikirudi kwenye mada.

Kuna uwezekano mkubwa Tanzania pia inahusika katika biashara ya madawa ya kulevya nchi jirani ya Kenya. Hii inatokana na alichokisema dereva wa raia wa kenya aliyewakaribisha Two Brothers wakati akihojiwa na Mohamed Ali. Dereva huyo alisema katika kusanyiko lilowahusisha maafisa wa ikulu ya Kenya mkuu wa CID , NSIS nakadhalika ma 'board guard' wawili kutoka Tanzania walikuwepo pia.

Ushahidi wa tuhuma hizi unapatikana katika clip hii>>>Jicho Pevu: Parawanja la Mihadarati Part 3 & 4 - YouTube

Tazama na kusikiliza kipande cha dakika 59:18 mpaka 59:21 utapata ushahidi huu.
 
...Mwai Kibaki naye aliwagwaya....wauza mihadarati...kama marais wengine waliotangaza kuwajua wauza mihadarati lakini wakashidwa kuwasema na kuwachukulia hatua. Kibaya zaidi, Kibaki, alivunja mapatano na maaskari aliowatuma kufanya uchunguzi wa wahusika wa kuingisa mihadarati nchini mwake.Mapatano hayo yalikuwa kwamba maaskari hao hawataingiliwa kwenye uchunguzi wao lakini haikuwa hivyo.

Maaskari hao ambao walikaribia kukamata ushahidi wa kuwatia nguvuni washukiwa muhimu wa mihadarati nchini humo walilazimishwa kuacha kazi yao hiyo bila maeleze yanayoeleweka...na hata maaskari ambao walitaka kufanya uchunguzi huo baada ya wale maaskari Kibaki, waliuliwa...


Hili kudhibitisha tuhuma za udhaifu dhidi ya Kibaki.....fuatilia mahojiano ya Mohamed Ali na Jarso Gadana,aliyekuwa SSP wa Polisi ya Kenya, ambaye alikuwemo kwenye kikosi kazi cha Kibaki kuanzia dak 07:56 kwenye link hii>>>>Jicho Pevu: Parawanja la Mihadarati Part 3 & 4 - YouTube

....Yawezekana mauaji ya wanausalama wetu yanayotokea kwa sababu zisizoeleweka ....za weza kuwa ni harakati za kujinasua kwa wahusika wa mihadarati ...huku mambo ya siasa yakitumika kama kinga tu.
 
Hii kitu ndio imehamia Tanzania baada ya viongozi wetu ku-join the business
 
Hii kitu ndio imehamia Tanzania baada ya viongozi wetu ku-join the business
Waweza kuwa sahihi...maana wale mabodigadi waliosemwa....post # 4 ya huu uzi yawezekana walienda kuratibu....simna kumbuka muvumenti za lidaz wetu walivyokuwa shadadia Kinyatta akamate ikuru.
 
Nimelazimika kusogea mbele zaidi ya pale kabindi alipoishia.....

Mnamkumbuka Profesa G. Saitoti (R.I.P)...aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Kenya ambaye alifariki kwa ajari ya ndege akiwa na naibu waziri wake Orwa Ojode( R.I.P) marubani wawili na walinzi wao? Kabla ya kifo chake aliomba apewe siku saba ili aandae ripoti ya wauza mihadarati na ataiweka hadharani... bahati mabaya sana hakutimiza azma yake hiyo. Inasemekana Saitoti alitaka hasa aueleze umma wa wakenya namna Two Brothers walivyokuwa "wameiteka Kenya". Kwa maelezo zaidi juu ya tukio hili gonga link hii hapa>>>https://www.jamiiforums.com/kenyan-...nister-george-saitoti-reported-killed-32.html

Mohamedi Ali wa KTN aliandaa kipindi kingine alichokipachika jina la Ghuthuru ya Saitoti...akilielezea kilichotokea kabla na baada ya ajari kutokea. Pia aligusia kwa unda namna uchunguzi wa ajari hii ulivyochakachuriwa na NSIS wakishirikiana na Dkt nadhani wa serikali ya Kenya J. Odwor.

Ghururi ya Saitoti ama kwa kiswahili Uchunguzi wa kifo cha Saitoti wa Mohamed Ali ni hii>>>>Jicho Pevu: Ghururi ya Saitoti - Uchunguzi wa kifo cha Saitoti - YouTube

Katika ripot hii Tanzania pia imetajwai fuatilia link hiyo juu kuanzia dakika ya 42:59 na baadaye anzia saa 1:19:15
 
Huyu Mohamed Ali anastahili nishani (Award). Kwa kweli hana mpinzani, sisi hapa Tanzania waandishi wa habari za uchunguzi wanamwagiwa tindikali na kufungia kazi zao - Said Kubenea, MwanaHalisi.
 
Mwandishi gani hapa Tanzania anathubutu kufanya hili? Zaidi ni kushabikia kinachosemwa na wanasiasa maarufu tu fulani kasema fulani fisadi chama fulani fisadi bila kuweka a critical evidence kama huyu Mh. naungana na MpangoA kuwa jamaa anahitaji award. Namkumbuka mwandishi alieylishwa sumu baada ya kuvumbua wizi wa vifaru kule loliondo na kuuweka wazi, nakumbuka Mshana wa Guardian alivyowekwa ndani mara kadhaa na mwisho jumba yake kupigwa bomu kisa haya mambo ya wizi na madawa mwisho mhusika alijiua kwa kujitumbukiza ziwa victoria na ikawa mwisho.

Jamaa anaposema tunaposikia sisi huhakikisha ni somo kubwa kwa waandishi wetu na hasa sisi wa JF tunaodakia tu wakati haohao wanasiasa tunaowashabikia ndiyo hao ni majizi, ni wauza unga, mafisadi wa ukweli lakini hujificha katika udhaifu wetu wa kufuatilia mambo kwa kina. MUNGU MWENYEZI WABARIKI JICHO PEVU NA UWAONGOZE KATIKA KAZI ZAO.
 
Huyo Mohammed Ali ni kiboko...nilimvulia kofia katika ile makala ya Zilzala ya Westgate...hakunaga...
 
Back
Top Bottom