Chunusi yaua kijana Tanga

Baba jayaron

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2015
Posts
4,324
Reaction score
5,933
Habari wanajamvi,

Leo nimekuja na habari ya kweli na kusikitisha iliyonipa maswali magumu ambayo ni haya kwanza Chunusi wa baharini ni jini au mnyama? Je sayansi inatambuaje maiti iliyouliwa na Chunusi?

Basi habari yenyewe ni hii niliyoipata kwa stuff mwenzangu kuhusu msiba uliotokea kwa jirani yake mtoto aliekua akifanya kijiwe na wenzake nje ya fensi ya jirani yangu.

Wiki moja kabla ya kifo kijana huyo aliuza simu yake akidai mitandao inamfanya aangalie vitu vya ajabu, Jumapili siku ya tukio alimuomba radhi mama yake kwani walipishana itikadi kipindi cha uchaguzi mama akiwa CCM mtoto shabiki mnazi wa Lowassa na chama kubwa CHADEMA (UKAWA) tofauti hii iliwafanya wapishane kiasi flani hivo siku hio alimuomba msamaha mama yake nakumwambia hawatapishana tena kwasababu ya siasa.

Jamapili hio hio aliamua kufua nguo zake zoote na kubaki na nguo alioivaa tu huku akitangaza hataki uchafu maishani mwake, mama yake kwa furaha ya kuombwa msamaha na mwanae akaamua kumpikia pilau mwanae maana amejirudi.

Wakati shuhuli zote zinaendelea kijana aliamua kumtania mama yake nakumwambia apunguze kukopa lasivo kama yeye hatokuwepo hatokua na mtu wakumsaidia kulipa na hivo atamkunbuka sana hivo ajiandae kuacha kukopa.

Baada yakumaliza kufua na mama mtu alikua anafunikia pilau Jumapili hio kijana akaamua kwenda kwa washkaji zake mara moja mama alimsisitiza asichelewe, kufika tu kwa wenzake wakamwambia walikua wanamfuata ili waende bichi kuogelea kijana alikataa katu katu akasema leo hajisikii kutoka anataka ashinde nyumbani tu.

Kwakua wenzake walikua wawili walimzidi ushawishi ikabidi aende bila hata kula kufika kituo cha basi wanakutana na rafki yao mwngine nae akamsisitiza asiende kwani siku hio si nzuri, alimsihi sana jamaa akataka kukubali lakini wale wawil walishinda tena.
Kufika bichi kijana akawaambia wenzake kwamba leo anaweza kurudi nyunbani bila nguo, wenzake walipuuzia kwani walijua ni utani wake maana ni mtu mtani sana.

Wakaanza kuogelea baada ya mda hawamuoni mwenzao wakazani labda ameondoka nyumbani na kibukta kama alivosema hatorudi na nguo nyumbani, kufika geti la bichi anaulizwa mlizi kama kamuona akitoka akasema hapana kufika nyumbani kwao pia hajafika na nguo wanazo mkononi.

Ikajaa hofu nyumbani wakijua kesha zama, wakatoa taarifa polisi na wao wakaamua kwenda baharini alipokua akiogelea waone kama watauona japo mwili, na kweli waliuona ukielea wakautoa uli mwili ukiwa na matope miguuni tu macho yamemtoka na mikono ngozi kama alikua anashindana na mtu lakini akiwa hajavimba kwamba alikunywa maji, mpaka anazikwa macho yakiwa wazi yamekataa kufumba.
Inasikitisha ila inaniacha na maswali nashindwa kuamini ni kweli chunusu?

Mwenye uelewa na haya karibu utusaidie
 
Habari mbaya hii...Pamoja na mambo mengi ya ajabu yaliopo kwenye maji ila maji yenyewe tu mimi nayaheshimu sana na si kwa ajili nimezaliwa kaskazini pasipo na bahari hapana ila hata yale ya mtoni mi sitakagi urafiki nayo kabisa, One mistake two goals.
 
Hebu Mshana Jr. Njoo utupe darasa pana kuhusu hili,maana hata mimi huwa linanitatiza sana.
Zaidi hii story imenisikitisha sana,I wish if I could turn back the time kumuokoa huyu kijana!!!!
Pole sana kwa mama mzazi,pilau lako la furaha limegeuka la msiba!
So sad!
 
Rest in Peace. Lakinin Hii kitu inaitwa chunusi ilinifanya kushindwa kukatiza barabara fulani enzi za utoto tukiaminishwa kwamba njia hizo zina chunusi.

Lakini cha ajabu hakuna aliyewahi kuniambia chunusi ni nani?
 
Tanga ni kubwa,hili tukio limetokea wapi na mkazi wa mtaa gani?
 
naogopa ya baharini sana
na mtoni nikimfikilia mjomba mamba hamu sina kabisa hata ya kuogelea
na ndo mana mpk sasa sijui kuogelea
pole yangu
 
Chunusi ni aina ya Jini ambalo huwa mara nyingi anaishi kwenye majini kwa maana we can say ni spirits amazo zinaishi majini

hawa spirits wamegawanyika kwa maana ya good spirits na evil spirits

evil spirits ni spirits ambazo zinaleta madhara kama ukame, njaa, mafuriko na mauaji

chunusi ni evil spirits ambao kwa hapa kwetu wanaishi kwa kunyonya damu za viumbe wengine inaweza kuwa mnyama au binadamu

sie Tanzania ubishi wetu na "kuelimika" tunajifanya HATUAMINI kuwa kuna kitu kama chunusi lakini chunusi wapo kila sehemu Duniani na kila eneo kuna jinsi wanavyomuita
MFANO:




tujika kwa Ainu Mythology kwa wajapani huwa wanamwita Amemasu huyu amemasu anaishi katika ziwa Mashu huko hokkaido



Australia kuna Chunusi wao wanamuita Eingana au mother of all na umbo lake huyu ni kwamba hana PAPUCHI



Wenzetu wachina wana mtu anaitwa GONG GONG ambaye huyu alikuwapo tokea
before 221 BCE)


wa eGypt na wao wanaye anaitwa Knum





huyu nitakuja kumwelezea vizuri siku nyingie kwani wamemjengea hadi Temple huko Elephantine na kizazi chake huyu amewazaa kina Seth, Neith, Isis mpaka kizazi cha mwisho kina Kebechet



tukija wagiriki ndio balaa maana wana kina Ladon, Kina Pan etc hawa wote ni chunusi wa nchi hizo


Hawai yupo wanamwita Kalanoa au Tangaroa


ndugu zangu wahindi pale Ganges River kuna GANGA yupo pale ametulia




Zimbabwe hapo jirani kuna Nyami Nyami... yaani huyu undava undava tu kwake



Wanaigeria wanamjua sana OSHUN ambaye ni chunusi maarufu sana

 
Dah hii story mi nilklikuepo huyo alikuwa anaruka kwenye bot zilizopaki yatch club waliingilia tanga bathing club jina maarufu beach ya waswahili mimi nilikuepo raskazone swiming club ni karibu sana na huyo alipatikana jumatatu saa saba mchana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…