Chunyu Ruangwa, Lindi: Msaada wa pembejeo za korosho unapewa chupa moja na nusu

Chunyu Ruangwa, Lindi: Msaada wa pembejeo za korosho unapewa chupa moja na nusu

Shindu Namwaka

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2014
Posts
4,911
Reaction score
3,083
Sina maneno mengi Swali langu kwa Mheshimiwa waziri wa kilimo mimi nina mikorosho zaidi ya 40 wengine wana mikorosho zaidi ya 100 lakini unapewa chupa moja ya salfa ya maji na chupa moja ya wadudu mnagawana nusu kwa nusu watu wawili. Kama lengo kumsaidia mkulima chupa moja na nusu itamsaidia kweli?
 
Sina maneno mengi Swali langu kwa Mheshimiwa waziri wa kilimo mimi nina mikorosho zaidi ya 40 wengine wana mikorosho zaidi ya 100 lakini unapewa chupa moja ya salfa ya maji na chupa moja ya wadudu munagawana nusu kwa nusu watu wawili kama lengo kumsaidia mkulima chupa moja na nusu itamsaidia kweli?
Kuna mambo ni upuuzi mtupu.
Ni kwanini Serikali badala ya kugawa Bure, wasitengeneze mazingira hizi Pembejeo na madawa vipatikane kwa gharama ambazo hazitamuumiza Mkulima?

Huku wa Korosho wanagaiwa Sulphur bure, na wanalalamika haiwatoshi. Sisi wa mahindi hamna anayetujali. Ni kwanini hizo pesa wanazotumia kununulia Sulphur wasii subsidize kwenye Pembejeo zote ili kuleta unafuu kwa wakulima wote?

Hii double standard ambayo hata Mlengwa anailalamikia inamnufaisha nani hasa?
 
Hizo sulphur hawapati bure. Msimu uliopita ni kama serikali waliongea na buyers wadeduct TZS 110 kwa kila kilo wanapotender kununua Korosho na hiyo 110 walichukuwa serikali kwaajili ya kuwalipa wazabuni waliokopesha sulphur kwa wakulima wote.

Tatizo hakuna transparency, maana hatujui wazabuni walikuwa wanadai shillingi ngapi wala hatujui hizo 110 zilizokatwa ziliraise kiasi gani na je kuna baki au surplus kwenye hizo pesa zilizokatwa baada ya wazabuni kulipwa.

Serikali pia haina nia ya dhati kumsaidia mkulima maana mpaka sasa Sulphur iliyopo nchini haitoshi na ndio muda hasa wa kupulizia mikorosho.
 
Sina maneno mengi Swali langu kwa Mheshimiwa waziri wa kilimo mimi nina mikorosho zaidi ya 40 wengine wana mikorosho zaidi ya 100 lakini unapewa chupa moja ya salfa ya maji na chupa moja ya wadudu munagawana nusu kwa nusu watu wawili kama lengo kumsaidia mkulima chupa moja na nusu itamsaidia kweli?

Halafu utasikia serikali wanajisifia kuwa wameweka bajeti kubwa ya kilimo ili kuwafaidisha wakulima. Mimi baada ya kugundua mazao yenye mtazamo wa kusaka sifa za kisiasa ni kupotezeana muda, nimeachana kabisa na hayo mazao. Sina muda wa kuendekeza siasa za kitapeli kwenye pesa zangu.
 
Huyu bashe akiendekeza utapeli wa wizara ya kilimo ya Toka Tanzania tunapata uhuru ,ahesabiwe kwenye fungu la wasiorudi bungeni 2025, Jana nimeshangaa zile pikipiki zimewekwa maonyesho ya nanenane sijui,hii wizara ni aibu kama Hadi Leo tunazalisha alizeti ya kutosha kutengeneza koroboi moja ya mafuta ya kupikia
 
Back
Top Bottom