Chuo cha afya Ngudu kimetelekezwa na serikali

mandago shululu

Senior Member
Joined
Mar 24, 2013
Posts
125
Reaction score
36
Chuo cha Afya ngudu ni miongoni mwa vyuo vikongwe vinavyoongozwa na serkali kwa huduma zote,Lakini kwa sasa chuo hiki kimetelekezwa na serikali kwa huduma zote zinazowahusu wanachuo wa hapo,baadhi ya matatizo yanachokikumba cho hicho ni pamoja na.

1.Ukosefu wa chakula
2.Mazingira mambaya,nyasi ni ndefu kama umeingia mbugani.
3.Hakuna sehemu ya kutupia uchafu
4.Vyoo ni vichafu
5 Sehemu ya kuchotea maji ni chafu sana.
6.Wasichana kujiuza ili wapate fedha ya chakula.
7.Uongozi wa chuo kutowapa Apdate za taarifa kutoka serikali/uongozi wa chuo uko mbali na wanachuo.

Hayo ni baadhi tu ya matatizo ambayo hukikabiri chuo cha Afya ngudu,Serikali iliwataka wanachuo wajitegemee kwa chakula ambapo waliambiwa kwamba wawewanatumia Tsh2500 kwa siku,ili pindi fedha zikipatikana watarudishiwa kitu ambacho hakiwzekani kabisa,hapa tujue kwamba kuna wale wanaotoka kwenye familia masikini watazitoa wapi hizo pesa? Kwa maisha ya Ngudu huweza ukatumia Tsh 2500 kwa siku ukimanisha milo mitatu,chai,mchana na usiku,chakula cha bei ya chini kwa ngudu ni 1500 wali maharage/ugari maharage,hapo bado haujanywa chai na mlo mwingine wa tatu,je 2500 kwa siku inatosha?

Bajeti ya Widhara ya Afya ya 2012-2013 inajipambanua wazi kwa matumizi ya kugharamia vyuo vyote vya serikali sasa hoja ya kusema kwamba Serikali haina pesa inatoka wapi?

Wakati wakisema hawana pesa ikumbukwe kwamba serikali hii hii inalipa zaidi ya Tsh300,000,000/= kwa siku kwa ajiri ya kuwalipa wajumbe na wabunge wa bunge la katiba,ifikie hatua hizi pesa zituume na tutoe huduma kwenye sekta zingine.

Suala la kusema kwamba watumie pesa zao halafu watarudishiwa hiyo ni danganya toto tu,hapa hakuna pesa itakayorudishwa kwani hatuwajui? Kuna wanachuo wanaomaliza mwaka huu ni vigumu kukaa unafatilia fedha wakati muda huo utakuwa mbali tu.

Hli hii imewalazimu wanafunzi hasa wa kike wajikite kwenye anasa ili kuweza kujikimu na kupata walau pesa ya chakula kitendo ambacho kinahatarisha afya za dada zetu.

Tunaiomba serikali iweze kurudisha huduma hii chuoni hapo ili kuondokana na kuzuka kwa vitendo visivyo vya lazima kwa wanafunzi kama vile udokozi na umalaya,tunakoumba sana waziri wa Afya ulifanyie kazi jambo hili,vile vile pesa ambazo wanachuo wametumia waweze kurudishiwa haraka iwezekanavyo kwani tunajua pesa zipo.
Unaweza ukajionea picha mballi mbali za maeneo ya chou hicho za kutia aibu kwa kuingia facebook na kuandika Mandago shululu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…