Tumekuwa tukisikia hapa Duniani hasa Tanzania kuwa huwa kuna degree za bure na wengine wamekuwa wakisema kuna degree za chupi, lakini sijawai kusikia au kuona watuhumiwa wakikiri kufanya uhalifu kabisa hadharani!
Your browser is not able to display this video.
Chuo cha Ardhi ni chuo kizuri lakini ikifika hatua ya watu kisa tuu mapacha wanaweza kufanyiana mitihani na wana kiri hadharani kuwa walifanyiana mitihani tena ya supplimentary basi ujue hii ni hatua kubwa na dharau kubwa sana kwa taasisi hasa ya Elimu ya juu na inayo aminika.
Hawa mabinti wanasema waliweza kufanyiana mitihani na walimaliza chuo kikuu Ardhi(ARU) mwaka 2021 hakuna aliyegundua na sasa wanakwenda hadharani kusema kuwa waliweza kufanya hivyo ni wazi dharau sana kwa taasisi hii ya Elimu na inathibitisha kuwa taasisi hii haiko makini na kuna walakini kwenye hutoaji wa Elimu.
Watu wana hangaika sana kupata elimu halafu watu wanaidhalilisha elimu kiasi hiki, hii ni aibu kwa chuo cha Ardhi na Wizara ya Elimu pia.
Watu wengi wamekuwa wakitilia mashaka sana Elimu zetu hasa utoaji wake na sasa ni wazi wahalifu wameanza kutoa ushahidi wa mashaka kwenye hizi degree zilizojaa mtaani.
Ni matuamaini yangu taasisi itachukua hatua kali dhidi ya uhalifu huu wa kielemu uliofanywa na hawa mapacha na kwenda kukiri hadharani kwenye chombo cha habari Wasafi FM.
Mzumbe pia morogoro kulikuwa na mapacha wa kike wanafanyiana mtihani
Mmoja kichwa anajua hesabu sana anasoma kozi ya BAF mwingine kilaza hajui hesabu anasoma kozi ya marketing
Hivyo yule kichwa akawa anambeba pacha wake maana walikuwa kozi tofauti pepa zinapishana ratiba. Mpaka UE anamfanyia.
Siku ya pepa za hesabu, accounts, na economics pacha kilaza alikuwa anafanyiwa na pacha kichwa.
Inasemekana mpaka necta form 6 alimfanyia pacha wake pepa ya Basic applied Mathematics maana pacha kichwa yeye alikuwa hafanyi BAM yeye alikuwa anafanya pepa ya Pure Mathematics ambayo ilikuwa siku tofauti.
Hao mapacha Wanafanana kweli kweli bila kuwazoea sana huwezi watofautisha
Duu hivi vyuo jamani kwa hiyo kumbe watu wanaweza fanyiana mitihani kwakuwa ni mapacha? Ina maana kila kitu hadi registration number wana fanana? Ili la kwenda kwenye vyombo vya habari na kukiri ni fedheha kubwa sana kwa chuo!
Ni warembo lkn hawana hekima wala busara, maana hekima ni kuliweka kila jambo mahala pake,,,sasa kama hawajui walichofanya ni kosa na kama haitoshi wanajisikia sifa kuongea hadharani,basi ni wapuuzi Sana
Duu hivi vyuo jamani kwa hiyo kumbe watu wanaweza fanyiana mitihani kwakuwa ni mapacha? Ina maana kila kitu hadi registration number wana fanana? Ili la kwenda kwenye vyombo vya habari na kukiri ni fedheha kubwa sana kwa chuo!