Chuo
Habari zenu wakuu,
Sisi Wanafunzi tunaoendelea na mwaka wa masomo ukitoa wale wa Mwaka wa Kwanza ambao ni wapya hapa Chuo cha DIT (Dar es Salaam Institute of Technology) tuna changamoto ya Chuo kutotuma taarifa zetu kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)
Tulifungua Chuo wiki tano zilizopita, utaratibu ulivyo tulitakiwa kupata matokeo kisha taarifa hizo za matokeo zitumwe HESLB ili tuweze kupata mikopo yetu ikiwemo fedha za kujikimu “Boom”.
Baada ya kupiga sana kelele hatimaye Chuo kikatoa matokeo lakini taarifa hizo hazijatumwa HESLB mpaka sasa (leo Novemba 21, 2024) hali hiyo inansababisha tushindwe kuingiziwa fedha na tunapoulizia ngazi ya Chuo kupitia kwa Waziri wa Mikopo, anatupa majibu ya ovyo.
Awali, Chuo kilidai kuna Wanafunzi ambao matokeo yao siyo mazuri, sawa vipi kuhusu sisi wengine ambao hatuna matokeo mabaya, mbona taarifa zetu hazitumwi?
Hali hii imesababisha wengi wetu kuishi kwa tabu hapa Mjini, masomo yanachanganya lakini hatuna mwelekeo mzuri kwa kuwa hatua fedha na tunaishia kuwa na madeni Mitaani.
Baadhi ya wenzetu kutoka mikoani wamekwama kuja mpaka sasa, hawajaingiziwa hela, wanashindwa kuelewa wakija town wataishije.
Mamlaka za juu za chuo zimekaa kimya bila kutupa ufafanuzi, tunaumia, inasemekana wao Chuo hawana muda wa kuharakisha taarifa hizo kwa kuwa utaratibu wa wao kupokea ada zetu kutoka HESLB ni tofauti kidogo ndio maana wanaacha sisi tuendelee kuteseka kwa kuwa hilo haliwagusi wao moja kwa moja.