KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 82
- 150
Sisi Wahitimu wa ngazi ya Shahada wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kutoka kampasi zote wa Mwaka wa Masomo 2023/2024 tunakabiliwa na changamoto kubwa ya ucheleweshaji wa vyeti licha ya kufuzu masomo.
1. Kukosa Fursa za Kazi: Ucheleweshaji wa vyeti unatuzuia wahitimu kuomba nafasi za ajira zinazohitaji cheti kama kigezo muhimu, hali inayowaweka katika changamoto za kifedha na kijamii.
2. Kucheleweshwa Maendeleo ya Kitaaluma kwa wanaohitaji kuendelea na masomo: Wahitimu wanakosa nafasi za kujiendeleza kielimu katika shahada za juu ndani na nje ya nchi, jambo linalozorotesha mipango yao ya maisha.
Natoa wito kwa IFM na mamlaka husika kuchukua hatua za haraka kutatua changamoto hii ili kulinda maslahi ya wahitimu hawa.
Vyeti vilitakiwa kutoka tangu Desemba 2024 lakini sasa ni Februari 2025 hakuna majibu yaliyonyooka, kila tukienda kuuliza tunaambiwa wanashughulikia.
Tetesi zilizopo ni kuwa Chuo kinadaiwa na Mzabuni wa Serikali, kuna malimbikizo ya malipo hayajafanyika, hivyo Mzabuni amegoma kuwapatia vyeti, kama hivyo ni kweli basi tunaumia sisi ambao hatuhusiki na hayo makosa ya Uongozi wa Chuo.
RAIS WA WANAFUNZI IFM
JamiiForums imewasiliana na Rais wa Wanafunzi wa IFM, Fabian Cornelius Mkondo kuhusu hoja hiyo, amesema:
“Ni kweli nilipata malalamiko hayo, siyo jambo gani, nimelifikisha kwa viongozi wa chuo wanaohusika wanalishughuliki, mimi pia nalifanyia kazi kwa upande wa levo yangu.
“Chuo kipo kwenye kipindi cha mitihani, ndio maana ‘focus’ ipo huko sana lakini naamini Chuo kitashughulikia na suala hilo litamalizika.”
Jitihada za JamiiForums kuutafuta Uongozi wa Chuo cha IFM zinaendelea.