Chuo cha Kampala hakijatupa ‘refund’ za Mwaka 2023, wanadai wanazirejesha Bodi ya Mikopo, kama kweli HESLB toeni tamko

Joined
Sep 23, 2024
Posts
64
Reaction score
43
Sisi Wahitimu wa Shahada katika Chuo cha Kimataifa Kampala kilichopo Gongo la Mboto, Dar es Salaam hatujapewa malipo yetu yaliyozidi (refund) kutoka kwenye fedha tulizokuwa tunalipiwa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).

Wakati tukiwa mwaka wa pili (Mwaka 2023) kuna wengi wetu tulilipa sehemu ya ada kwa fedha zetu wenyewe kwa lengo kuwa malipo ya Bodi ya Mikopo yakiin gia chuo kitafidia na kuturejeshea fedha zaetu.

Tangu wakati huo hadi tulipohitimu Desemba 2024 Chuo hakikuwa kimerejesha fedha zetu hizo zilizozidi, kwa darasa letu tu ambao tunadai ni zaidi ya 200, sijui kwa madarasa mengine

Kila mmoja wetu anapoenda kuulizia kuhusu refund anajibiwa kuwa fedha hizo zitarejea Bodi ya Mikopo kitu ambacho kiuhalisia tunajua sio cha kweli.

Kwani utaratibu ulivyo walitakiwa kutupe fedha hizo kisha sisi tutaanza kuilipa Bodi pindi tutakapopata ajira, sasa suala la kuwa wanazirejesha Bodi sio la kweli kwa kuwa tumeshachukua vyeti, wanasubiri baada ya muda tukienda watukane kuwa kama tumeshachukua vyeti inamaanisha hakuna tunachodai wala kudaiwa

Tunaomba Bodi kama kweli fedha zimerejea kwao watoe tamko ili tujue tutakapoanza kuwalipa basi wao wakate sehemu ya fedha hizo.

Kiwango tunachodai kwa kila mtu ni tofauti kulingana na alivyolipa, wapo wanaodai kuanzia Sh laki tatu hadi laki saba, sasa chukua hiyo fedha mara 200 utajua nini kinaendelea.

Mbona wenzetu wa SUA wao tumewasiliana nao wamesema wamerejeshewa fedha zao zilizozidi? Kwanini Kampala iwe tofauti?
 
Sisi Wahitimu wa Shahada katika Chuo cha Kimataifa Kampala kilichopo Gongo la Mboto, Dar es Salaam hatujapewa malipo yetu yaliyozidi (refund) kutoka kwenye fedha tulizokuwa tunalipiwa na Bodi ya Mikopo (HESLB)

Wakati tukiwa mwaka wa pili (Mwaka 2023) kuna wengi wetu tulilipa sehemu ya ada kwa fedha zetu wenyewe kwa lengo kuwa malipo ya Bodi ya Mikopo yakiin gia chuo kitafidia na kuturejeshea fedha zaetu.

Tangu wakati huo hadi tulipohitimu Desemba 2024 Chuo hakikuwa kimerejesha fedha zetu hizo zilizozidi, kwa darasa letu tu ambao tunadai ni zaidi ya 200, sijui kwa madarasa mengine

Kila mmoja wetu anapoenda kuulizia kuhusu refund anajibiwa kuwa fedha hizo zitarejea Bodi ya Mikopo kitu ambacho kiuhalisia tunajua sio cha kweli.

Kwani utaratibu ulivyo walitakiwa kutupe fedha hizo kisha sisi tutaanza kuilipa Bodi pindi tutakapopata ajira, sasa suala la kuwa wanazirejesha Bodi sio la kweli kwa kuwa tumeshachukua vyeti, wanasubiri baada ya muda tukienda watukane kuwa kama tumeshachukua vyeti inamaanisha hakuna tunachodai wala kudaiwa

Tunaomba Bodi kama kweli fedha zimerejea kwao watoe tamko ili tujue tutakapoanza kuwalipa basi wao wakate sehemu ya fedha hizo.

Kiwango tunachodai kwa kila mtu ni tofauti kulingana na alivyolipa, wapo wanaodai kuanzia Sh laki tatu hadi laki saba, sasa chukua hiyo fedha mara 200 utajua nini kinaendelea.

Mbona wenzetu wa SUA wao tumewasiliana nao wamesema wamerejeshewa fedha zao zilizozidi? Kwanini Kampala iwe tofauti?

Mnashindwa vipi kwenda bodi ya mkopo kuuliza Tena mpo barabara moja
 
Kwanza pole hicho chuo huwa kina ada ndefu aisee sikujua nimejua mwaka huu!
Anyway ushauri wangu ni mjiunganishe mfungue kesi ya madai hii itasaidia nyie kupata haki yenu
Tujifunze Kutumia sheria kupata haki zetu
Kila la kheri mshangazi mdogomdogo mi Niko hapa gym napiga tizi
 
Back
Top Bottom