Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mkuu wa Chuo cha Igabiro Training Institute of Agriculture, Sadoki Stephano ameelezea madai ya kuwa kuna changamoto ya Wanafunzi waliohitimu chuoni hapo kutopata vyeti huu ukielekea kuwa mwaka wa pili.
Amesema kilichotokea ni suala la kimfumo ndani ya Mamlaka ya Serikali na linashughulikiwa.
Awali Mwanachama wa JamiiForums.com alisema Chuo hicho kilichopo Wilayani Muleba hakijawapa vyeti wahitimu wa awamu mbili ikiwemo wao waliohitimu Diploma in Animal Health and Production, Februari 2023 na kuwa kila wanapofuatilia wamekuwa wakipiga kalenda.
Soma zaidi hapa ~ Chuo cha Kilimo cha Igabiro hakijatupa vyeti vyetu, miaka miwili tangu tulipohitimu, kila siku wanatuzungusha
CHUO CHATOA UFAFANUZI
Mkuu wa Chuo cha Igabiro Training Institute of Agriculture, Sadoki Stephano anaelezea:
Kwanza ifahamike kuwa Chuo chetu hakizalishi vyeti, Wanafunzi wamesajiliwa kwenye mfumo wa Kiserikali, wapo ambao vyeti vyao vinatoka NACTVET (Baraza la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi) na wengine vyeti vyao vinatoka Wizara kwa kuwa hapa tuna kozi ya Kilimo na Mifugo.
Wanaosoma Mifugo Vyeti vyao vinatoka NACTVET, ambapo matokeo yao yakishatoka yanapitishwa kwenye Bodi ya Wizara kisha vyeti vyao vinachakatwa.
Upande wa Kilimo matokeo yakishatoka, Wizara ndio inachakata vyeti na kuvitoa.
Hivyo, suala hilo la Vyeti sio sisi tu kuna vyuo zaidi ya Tisa ambavyo navyo havijapata vyeti.
Kwa sasa taarifa ni kuwa vyeti vipo kwenye mchakato na wanaweza kupata ndani ya mwezi kutoka sasa.
Kwa maana hiyo, suala hilo la Vyeti sio jambo la chuo ni ishu ya Kiserikali, hii changamoto haikuwemo huko nyuma, ni masuala ya mifumo ndio yamesababisha iwe hivyo kutoka katika masuala ya mifumo ya chuo.
Pia soma ~ Kagera: Chuo cha Kilimo cha Igabiro chasema Vyeti vya Wahitimu vimetoka na vinapatikana chuo