Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere inaonekana kinaongozwa kiaina na Mkuu wa Chuo aliyestaafu. Mkuu huyo mstaafu ni DR. J. Magotti. Alistaafu rasmi tarehe 05/01/2014 lakini hadi sasa anatumia rasilimali za Chuo kama gari na dereva kanakwamba bado yuko kazini. Mtu aliyemkaimisha ukuu wa Chuo anapokea maagizo kutoka kwake. Chuo hiki kina matatizo mengi na tuhuma nyingi sana ambazo hadi sasa hazijatatuliwa. Sisi wanafunzi tuko kama wakiwa maana hatuna haki na tunaonewa na baadhi ya walimu bila msaada wowote. Tunatoa wito kwa mamlaka husika kuiangalia Chuo hiki kwa jicho la pekee maana sasa kinaidhalilisha elimu ya nchi yetu. Chuo hiki pia kina Msajili wa Chuo aliyetakiwa kustaafu 17/01/2014 lakini bado yupo tuu kazini. Inasemekana amebadilisha umri kuwa amezaliwa 1959 badala ya 17/01/1954 kama taarifa zake zinavyoonyasha. Huyu Msajili ambaye pia ndio mkurugenzi wa utawala na fedha anatuhuma lukuki lakini yupo tuu bila kuchukuliwa hatua yoyoyte. Mtu alikaimishwa ukuu wa Chuo naye anatuhuma ya kughushi matokea ya wanafunzi. Hao ndio viongozi wa Chuo tuhuma chungunzima na Chuo kinazidi kupoteza umaarufu wake wa awali. Naamini mamlaka husika zitakinusuru Chuo hiki mikononi mwa mafisadi hawa wa elimu.