Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kinaongozwa kiaina na Mkuu wa Chuo aliyestaafu?

Uzalendi

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2013
Posts
221
Reaction score
15
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere inaonekana kinaongozwa kiaina na Mkuu wa Chuo aliyestaafu. Mkuu huyo mstaafu ni DR. J. Magotti. Alistaafu rasmi tarehe 05/01/2014 lakini hadi sasa anatumia rasilimali za Chuo kama gari na dereva kanakwamba bado yuko kazini. Mtu aliyemkaimisha ukuu wa Chuo anapokea maagizo kutoka kwake. Chuo hiki kina matatizo mengi na tuhuma nyingi sana ambazo hadi sasa hazijatatuliwa. Sisi wanafunzi tuko kama wakiwa maana hatuna haki na tunaonewa na baadhi ya walimu bila msaada wowote. Tunatoa wito kwa mamlaka husika kuiangalia Chuo hiki kwa jicho la pekee maana sasa kinaidhalilisha elimu ya nchi yetu. Chuo hiki pia kina Msajili wa Chuo aliyetakiwa kustaafu 17/01/2014 lakini bado yupo tuu kazini. Inasemekana amebadilisha umri kuwa amezaliwa 1959 badala ya 17/01/1954 kama taarifa zake zinavyoonyasha. Huyu Msajili ambaye pia ndio mkurugenzi wa utawala na fedha anatuhuma lukuki lakini yupo tuu bila kuchukuliwa hatua yoyoyte. Mtu alikaimishwa ukuu wa Chuo naye anatuhuma ya kughushi matokea ya wanafunzi. Hao ndio viongozi wa Chuo tuhuma chungunzima na Chuo kinazidi kupoteza umaarufu wake wa awali. Naamini mamlaka husika zitakinusuru Chuo hiki mikononi mwa mafisadi hawa wa elimu.
 
Kwa sifa iliyonayo Chuo hiki kwa sasa haimvutii mzazi kumpeleka Mtoto wake kusoma hapo, ina sifa mbaya ya ufisadi katika elimu, naamini itachunguzwa kupata ukweli.
 
Mbon unatuma uzi then unaji comment mwenyewe.

Kama course work imekaa vibaya, kaza buti ufaulu.

Kama umeliwa kichwa (disco) jipange upya, si lazima kila mtu asome.

Vinginevyo hakuna ulichopost.
 
kwahiyo unataka sisi tumung'oe uongozi wake au tukusaidie msaada gani??? hii ingetakiwa mjiorganize hapo chuoni wanafunzi ni jinsi gani ya kuuondosha uongozi mbovu ulioko madarakani nasi kutuletea huku JF,kwa mfano sisi UDSM tunachukua uamuzi sisi wenyewe wanachuo kama tukiona kuna sehemu hatujaridhishwa
 
Kwani hicho nacho ni chuo au ni training college kwa short course thn unapata cheti cha mahudhurio
 
Mbon unatuma uzi then unaji comment mwenyewe.

Kama course work imekaa vibaya, kaza buti ufaulu.

Kama umeliwa kichwa (disco) jipange upya, si lazima kila mtu asome.

Vinginevyo hakuna ulichopost.

Unamaanisha hayo si ya kweli? Usibishe bila kufanya utafiti, Chuo hicho ni kichekesho kwa sasa. Fanya uchunguzi mdogo tuu utapata ukweli.
 
Tusaidiane kuufikisha ujumbe huu kwa mamlaka husika ili ikinusuru chuo hicho kwa kuwaondosha hao mazandiki.
 
Mbon unatuma uzi then unaji comment mwenyewe.

Kama course work imekaa vibaya, kaza buti ufaulu.

Kama umeliwa kichwa (disco) jipange upya, si lazima kila mtu asome.

Vinginevyo hakuna ulichopost.

ha ha ha mkuu umempa kubwa lol
 
Unamaanisha hayo si ya kweli? Usibishe bila kufanya utafiti, Chuo hicho ni kichekesho kwa sasa. Fanya uchunguzi mdogo tuu utapata ukweli.

Kwa kawaida hata mtu akifukuzwa kazi mahali, hatakumbuka wema aliokuwa akipatiwa ikiwa ni pamoja na mshahara, atatukana kila mtu, atatoa lugha chafu nk.

Vivyo hivyo vyuoni, usitegemee mtu alikuwa hasomi, ameliwa kichwa ufikiri atakisema vizuri!

Kama mhusika hajafukuzwa, ajiweke hadharani!
 
Majibu yako kama ya mbia wa mafisadi wa Chuo hicho, unaongea tuu bila ushahidi. Haya yanayozungumziwa humu kuhusu Chuo hicho ni ya kweli pasipo shaka.
 
ha ha ha mkuu umempa kubwa lol
Huu ni mchango wako au unajiandaa, kama ni mchango wako kwa mada hii ni kujidhalilisha maana hapa ni kwa wafanya utafiti si kama maongezi ya vijiweni.
 
we unaonekana umeliwa kichwa jipange upya tu

Wewe ni Ziro, ubongo hamna kitu, huo ni mchango katika mada au mzaha. Ona aibu kuacha wenye mawazo kuchangia wewe uwe msomaji.
 
Majibu yako kama ya mbia wa mafisadi wa Chuo hicho, unaongea tuu bila ushahidi. Haya yanayozungumziwa humu kuhusu Chuo hicho ni ya kweli pasipo shaka.

Sina ubia wowote, hichi unachokifanya ni defamation, weka ushahidi! Sipendi mbwabwanya maneno, popote pale kwa interest binafsi.
 
Sina ubia wowote, hichi unachokifanya ni defamation, weka ushahidi! Sipendi mbwabwanya maneno, popote pale kwa interest binafsi.
Kama huna ubia toa hoja zenye ushahidi wa unachozungumzia. Chuo sasa ni Chuo cha Kumbukumbu ya mafisadi na kinaendeshwa kifisadi, ushahidi ni wazi fika pale muulize yeyote utapata ukweli.
 
We juha mbona mara kadhaa tulishasema kuwa haya yako ni majungu tuu...Leo unajifanya ni mwanafunzi ilhali tunajua wewe ni staff mzembe unayetarajia favours pasipo kufanya kazi.Umempigia kelele mzee wa watu mpaka kastaafu na sasa hata huko aliko bado unazidi kubwabwaja...Spend yourbtime wisely hizi kelele za JF zinazidi kuexpose umbumbumbu wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…