elivina shambuni
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 461
- 295
Chuo cha Usafirishaji (NIT) kitaanza kutoa mafunzo ya urubani ambapo tayari kimepokea Tsh. 48.9 bilioni kutoka Benki ya Dunia (WB) kwa ajili ya ununuzi wa ndege 3 za mafunzo, kujenga karakana, na hosteli.
Inaelezwa kuwa Jumla ya wanafunzi 10 wanatarajiwa kuanza mafunzo hayo kwa mwaka 2020/21.
Kufuatia hatua hiyo, Rais Dkt Magufuli ameahidi kutoa ndege nyingine mbili, kuuanga mkono jitihada za chuo hicho kuanza kufunza marubani.