DOKEZO Chuo cha SAUT kishughulikie Mfumo wa Matokeo kuna malalamiko ya chinichini kuwa ‘unachezewa’

DOKEZO Chuo cha SAUT kishughulikie Mfumo wa Matokeo kuna malalamiko ya chinichini kuwa ‘unachezewa’

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

MeVSMe

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2024
Posts
270
Reaction score
425
Katika jitihada zangu za kutafuta elimu ya juu kwa ngazi ya Uzamili, nililenga Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) – Mwanza, hata hivyo, kile nilichokutana nacho katika utafiti wangu kuhusu mazingira ya chuo na mfumo wake wa matokeo kimeniacha na maswali mengi kuhusu uadilifu wa mfumo wa elimu chuoni hapo.
IMG_20250107_091407_021~2.jpg

photo_2024-12-31_08-20-58.png

Hatua za Awali: Wasiwasi wa Mfumo wa Matokeo
Mtu mmoja kutoka chuoni hapo aliniambia "kuwa risk taker" ni muhimu, kwani matokeo ya wanafunzi mara nyingi huathiriwa na mfumo wa usimamizi wa matokeo wa chuo.

Mfumo wa awali, unaojulikana kama OSIM, ulisemekana kuwa na changamoto nyingi, ikiwemo mabadiliko ya ghafla ya matokeo. Mfumo wa sasa wa SIMS umekuwa thabiti, lakini bado kuna malalamiko kuwa unatumika vibaya, hasa dhidi ya wanafunzi wanaokinzana na watumishi wa chuo.
IMG_20250107_091407_460~3.jpg
Nikiwa na endelea na uchunguzi wangu, mtoa taarifa mwingine aliyesoma hapo Mwaka 2020 alinieleza kisa cha kuhuzunisha.
IMG_20250107_091406_840~2.jpg
Anadai wakati wa mwaka wake wa tatu, alitengeneza tangazo la kubuni kwa kutumia taarifa rasmi ya chuo kama sehemu ya mazoezi yake ya kuboresha ujuzi wa Graphics Design. Bahati mbaya, tangazo hilo lilikubalika kama halali na kusambazwa zaidi ya alivyokusudia.

Hatua zilizofuata zilikuwa kali, alisimamishwa kwa mwaka mmoja, lakini aliporudi, alifanya mtihani na kufaulu. Siku ya mahafali, jina lake halikuwemo kwenye orodha ya wahitimu, aligundua kuwa matokeo yake yamebadilika kwenye mfumo, ikionyesha masomo aliyopaswa "kurudia" au "kufeli." Mpaka sasa, hajawahi kupata cheti chake licha ya kusoma na kulipa ada kwa ukamilifu.
photo_2024-12-31_08-20-59.jpg

Mtoa taarifa mwingine ambaye ni mhitimu wa Mwaka 2024 Kada ya Sheria, alieleza matokeo yake ya somo la Argumentative Skills yalibadilika kutoka "A" hadi "B plain" bila maelezo yoyote. Anadai licha ya kufuatilia, hakufanikiwa kurekebisha matokeo hayo.

Nilipozungumza na Wanafunzi kadhaa waliopo sasa wanasema wamejifunza kushughulika na hali hii kwa kuchukua matokeo ya awali mara tu yanapotangazwa ili kuwa na uthibitisho wa matokeo yao halisi.

Biashara ya Matokeo
Changamoto nyingine kubwa ni uwepo wa watu wanaojitambulisha kama watumishi wa chuo na kuahidi "kusaidia" matokeo ya wanafunzi kwa malipo.

Wanafunzi wengi wanasema vitendo hivi vinatokana na udhaifu wa mfumo wa usimamizi wa matokeo, hali inayoongeza changamoto kwa wahitaji wa elimu ya juu katika chuo hicho.
IMG_20250107_091407_460~2.jpg
Je, Mfumo Utarekebishwa?
Changamoto hizi zimeacha athari kubwa kwa wanafunzi, wakiwa na hofu ya kuwa matokeo yao yanaweza kubadilishwa ghafla au kutumiwa vibaya kama adhabu. Swali linalosalia ni je, chuo kina mipango gani ya kuboresha mfumo wake wa matokeo ili kuhakikisha haki na uwazi kwa wanafunzi wake?

Kupata elimu ni haki ya msingi, na changamoto hizi zinahitaji kushughulikiwa kwa haraka ili kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora bila ku
hofia matokeo yao kuchezewa.

Ufafanuzi wa Chuo, soma hapa ~ Msemaji wa Chuo Kikuu cha SAUT ajibu madai ya mfumo wao wa Matokeo kuchezewa na baadhi ya watu, asema upo imara
 

Attachments

  • IMG_20250107_091406_879~2.jpg
    IMG_20250107_091406_879~2.jpg
    56.7 KB · Views: 6
  • IMG_20250107_091407_162~2.jpg
    IMG_20250107_091407_162~2.jpg
    60.2 KB · Views: 5
Back
Top Bottom