KERO Chuo Cha SAUT-Mwanza lipeni Fedha zetu tulizozidisha kwenye ada

KERO Chuo Cha SAUT-Mwanza lipeni Fedha zetu tulizozidisha kwenye ada

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

makachu Makachu

New Member
Joined
Jan 13, 2025
Posts
4
Reaction score
4
Chuo Cha Saut-Mwanza sisi wanafunzi tuliokwisha maliza masomo yetu kwa takriban miaka Sasa miwili tumekuwa tukiwadai Fedha ambazo tulizidisha, na baadae mkatupa maelekezo kuwa tuandike barua za kudai lakini mpaka sasa hakuna malipo Mliokwisha tulipa.

Tumefuatilia sana hakuna majibu. Kumbukeni enzi tunasoma, hamkuturuhusu kufanya mitihani mpaka tuwe tumekwishalipia, Sasa ikija upande wenu kufanya marejesho hamfanyi tatizo lenu liko wapi?

Hii Fedha ni Jasho letu ni haki yetu tunaomba mturejeshe au mnataka tuwafungulie kesi mtulipe na fidia Ndio muelewe kuwa Fedha ni halali yetu?

Jitafakarini huduma zenu haziridhishi. Chukueni hatua stahiki kuturejeshea Fedha zetu sisi wanafunzi ambao tunawadai kwa takribani miaka 2 na zaidi.

Tunawasilisha katika Hali ya upole hatupendi kuandika ila mnatufanya tuone kama hamjali. Tuoeni Fedha hiyo hata tufanye mitaji Ili kujikwamua au hamjui kuna changamoto ya ajira? Na zaidi baadhi ya ofis tukija huko uhasibu hamtupi majibu sahihi.

Mnataka tusafiri kutoka mikoni kufuatikia hili? Kila mara mnadai account zetu hazipokei ziko inactive hamshughuliki kwa wakati.

Uongozi wa Juu kama mnadhani ni uongo fuatilie mtaona kuwa suala hili ni kero kubwa sana kwa wanafunzi tunapomaliza chuo.

Yawezekana uhasibu hapo kuna shida barua tunaandika sana au kama hamtulipi mmeifanya yenu tuambieni Ili tujue Moja.!

Cc Chancellor & TEC & VC
Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom