KERO Chuo cha SAUT-MWANZA wanasumbua kutoa vyeti kwa wahitimu, pia wanachanganya matokeo

KERO Chuo cha SAUT-MWANZA wanasumbua kutoa vyeti kwa wahitimu, pia wanachanganya matokeo

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tupo kwenye sintofahamu, Chuo cha SAUT-MWANZA mpaka sasa hakijatupa Vyeti wahitimu wa Mwaka 2023.

Ukienda kufuatilia wanasema tusubiri wakidai vyeti havijafika, wakati huohuo wengine wamepata, sasa tunashindwa kuelewa wanatumia utaratibu gani wa kutoa vyeti.

Baadhi ya waliopata nao pia wamekutana na changamoto ya TRANSCRIPT kuchanganywa masomo mfano kwa waliosoma BAED (Bachelor of Arts with Education) unakuta wameandikiwa Kiswahili & Literature lakini transcript unakuta imeandikwa Geography & Linguistic.

Tunapata shida Watu tunatoka mbali kufuata cheti unakutana na changamoto za ovyo, inakera sana.
 
Hicho chuo mbn kinamalalamiko mengi, wana shida gani
 
Lipa ada acha visingizio warumi hawanaga kona kona no fee no school lipa ada we build the city of God
 
SAUT Mwanza
Chuo changu
Nimepata maarifa mengi hapo
 
Iko chuo n cha kisenge sn sio pakwenda kusoma hapo wana mambo ya ajabu mengi mno malalamiko yamezid
 
Back
Top Bottom