Chuo cha Ualimu Monduli wamaliza kozi maalumu ya Bridging bila wakufunzi kuwezeshwa

Chuo cha Ualimu Monduli wamaliza kozi maalumu ya Bridging bila wakufunzi kuwezeshwa

KALEBE

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2011
Posts
773
Reaction score
339
napenda kuwapa pole wakufunzi wa chuo cha ualimu monduli kwa kazi kubwa walioifanya ya kufundisha kozi ya bridging kwa muda wa miezi mitatu bila kulipwa chochote.

kozi kama kama hii kwa mujibu wa taarifa ni kuwa iliwahi kutolewa katika chuo hicho cha monduli na morogoro miaka ya nyuma na kwa morogoro inavyosemekana ilitolewa pia mwaka wa jana ambapo wakufunzi wa chuo hicho walilipwa kiasi cha shilingi 40,000 kwa siku japo napo halikuwa jambo jepesi kwani ulikuwa ni mvutano mkali sana hadi kutolewa kwa kiasi hicho cha pesa. viongozi wa wizara akiwepo aliyekuwa mkurugenzi msaidizi mafunzo waliwaambia wakufunzi hao ya kuwa watakuwa wanalipwa kiasi cha shilingi 10,000 kwa siku ndipo wakufunzi hao walipohoji uhalali wa malipo hayo kama hicho kiasi kinaendana na kiwango cha serikali baada ya mvutano kuwa mkali wizara wakaamua kutoa kiasi cha shilingi 20,000 kwa siku lakini pia wakufunzi hao waliendelea na mahojiano na uongozi wa chuo na wizara na mwisho wa siku wakaafikiana kulipwa kiasi hicho cha elfu arobaini.

kazi ilifanyika kwa muda wa miezi mitatu na wakufunzi hao walilipwa pesa yao yote kiasi cha shilingi milioni tatu na laki sita. kozi ilipoisha aliyekuwa mkuu wa chuo hicho ambaye kwa sasa ni mstaafu aliwaambia wakufunzi hao waliokuwa wanaendesha mafunzo hayo kuwa kozi hiyo itaendelea tena chuoni hapo mwakani kwa maana ya mwaka huu lakini cha ajabu mafunzo hayo yalipelekwa chuo cha ualimu monduli na taarifa kutoka chuo hicho zinasema ya kuwa mafunzo hayo hayakurudi tena chuo cha ualimu morogoro.

na hii yawezekana ni kwa sababu ya uvutano uliokuwepo kati ya wakufunzi wa chuo hicho na uongozi wa wizara pia kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa aliyekuwa mkuu wa chuo cha ualimu morogoro ambaye kwa sasa ni mstaafu alisema ya kuwa mafunzo haya ni ya miaka mitano ambapo yalianza mwaka 2011 na yanategemea kumalizika mwaka 2015 na hivyo yametengewa kiasi kikubwa tu cha pesa.

lakini cha ajabu na cha kusikitisha ni kuwa wakufunzi wa chuo cha ualimu monduli waliendesha mafunzo hayo bila malipo yoyote kwa muda wote wa miezi mitatu

hapa swali la kujiuliza ni je hiyo pesa ilikwenda wapi kama mafunzo ya aina hiyohiyo yalitolewa mwaka wa jana katika chuo cha ualimu morogoro na wakufunzi wake kulipwa pesa lakini cha ajabu mafunzo haya yameendeshwa monduli hawakupewa hiyo pesa?

tunaomba CAG akafanye pia uchunguzi katika suala hilo yawezekana tunaongelea wizi katika account ya escrow kumbe hii nayo yaweza kuwa escrow part II basi kama ni kula basi wangewapatia walau hata kiasi kidogo lakini hata hicho kiasi walikula chote. tunawaomba takukuru pia wakalifanyie suala hili uchunguzi ili kubaini ni akina nani waliohusika na huo ubadhilifu wa hiyo pesa.

cha kusikitisha ni kuwa wakufunzi hao walipohoji kuhusu namna gani ya kuendesha hayo mafunzo walijibiwa majibu makali kwamba yule ambaye hayuko tayari kufanya kazi aandike barua na ajaze fomu hivyo basi kutokana na hali ya uwoga wakufunzi hao waliogopa na kuamua kufanya kazi lakini walikuwa wanafanya kazi kwa unyonge kwani tayari walikuwa na taarifa ya kwamba wenzao wa morogoro mwaka wa jana walilipwa kiasi fulani cha pesa walipokuwa wanaendesha mafunzo kama hayo ambayo wao wanaendesha.

sote tunaanimi ya kuwa wale wote wanaofanya kazi wizara ya elimu kwa sehemu kubwa ni walimu au ni wakufunzi lakini cha ajabu wao ndio wanaowanyanyasa wenzao jambo hili kiukweli halikubaliki
wakati ni sasa wa kufanya mapinduzi ili kila mtu astahili kile ambacho anastahili hata kama ni kidogo
 
Back
Top Bottom