Chuo cha Ufundi Arusha: Teknolojia rahisi ya kuzalisha umeme

Chuo cha Ufundi Arusha: Teknolojia rahisi ya kuzalisha umeme

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Pamoja na jukumu la kuzalisha wataalamu wa fani mbalimbali, taasisi za elimu nchini zina nafasi kubwa ya kutatua changamoto kadhaa zinazolikabili taifa hili.
Kwa mfano, Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kimedhamiria kutumia wanafunzi pamoja na wakufunzi wao kubuni teknolojia rahisi itakayoweza kumaliza tatizo la umeme maeneo ya vijijini.
Mhandisi Urbanus Melkior, ni Mkuu wa Idara ya Umeme chuoni hapo, anayeamini kuwa wanafunzi wao kwa kushirikiana na wakufunzi, wanaweza kusaidia kutatua tatizo la umeme vijijini.
Katika kutekeleza hilo, anasema chuo hicho kimebuni mtambo mdogo wa kufua umeme ujulikanaokwa Kiingereza ‘Mini hydro Turbines’, unaotumia maji kwa kiasi kidogo.
“Mwaka 2011 kulikuwa na mgao mkubwa wa umeme. Watu walikuwa wanakaa bila umeme kwa kati ya saa nane mpaka 11, halihiyo ilitufanya tufikiri jinsi tutakavyoweza kufanya, ili kupata ufumbuzi wa tatizo la umeme,” anasema.
Anaeleza kuwa, baada ya hapo idara ya umeme ilishirikiana na idara ya mitambo hatimaye walifanikiwa kutengeza mtambo huo ambao umefungwa katika eneola Makumira wilayani Arumeru.
Melkior anasema kwamba, mtambo huo unaweza kuzalisha umeme kwa kutumia maji kidogo yanayopita kwenye mfereji. Kwa sasa takriban kaya 20 zinahudumiwa na umeme huo.
“Tunachofanya sisi ni kutengeneza mtambo na kwenda kuufunga, tukimaliza tunawaachia wanakijiji wanaoutunza,” anasema.
Anaeleza kuwa, teknolojia iliyotumika kuutengeza ni rahisi na inaruhusu mtu yeyote hata asiyekuwa mtaalamu wa umeme kuweza kuuhudumia mtambo huo.
“Mtambo ukishawekwa, kazi itakayokuwa inafanyika ni kufungulia maji yaje kwenye mtambo ama kuyapunguza, nyingine ni kupaka vilainishi tu, hii anaweza kufanya mtu yeyote,” anaeleza.
Mbali ya Makumira, mtambo huo piaumefungwa katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Morogoro, Iringa , Katavi, Njombe na Ruvuma.
Kichocheo cha uvumbuzi
Kubuniwa kwa mashine hiyo, anasema kulichochea ari ya wanafunzi kubuni vitu vingine zaidi kwa minajili ya kuisaidia jamii, kama anavyobainisha:
“Tuna takriban wanafunzi 18 kwenye idara yetu waliojitoa kuwa kama wavumbuzi. Hata baada ya muda wa masomo kumalizika wanabaki karakana kuumiza vichwa, ili waje na kitu kipya kitakachokuwa na manufaa kwa jamii.”
Anaongeza: “… sasa wamebuni kifaa cha kufukuza mbu, kifaa cha kutafuta madini chini ya ardhi na teknolojia rahisi ya kuzalisha vifaranga.”
Anasema kuwa, wamefanya hivyo kwa kuwa wanaamini mwanafunzi akipewa uhuru wa kufanya ugunduzi anaweza kufanya mambo makubwa.
Mhandisi Melkior anasema kuwa, ili kuongeza hali ya ubunifu, kuanzia mwaka huu kila mwanafunzi atatakiwa kubuni kifaa ambacho kikiuzwa kitaweza kurejesha gharama za mafunzo yake.
Anasema kuwa, hali hiyo itafanya pia wahitimu wa chuo hicho kuachana na dhana ya kutegemea ajira na badala yake watakuwa wanapenda zaidi kujiajiri kutokana na ubunifu wao.
Matunda ya mtambo
Justine Mungure, ndiye anayemiliki mashine hiyo ya kuzalisha umeme iliyofungwa kwenye eneo la Makumira. Anasema kwa kiasi kikubwa teknolojia hiyo imewasaidia kuondokana na mgao wa umeme.
Anasema kuwa, tangu kufungwa kwa mtambo huo Mei 2011, mpaka sasa hawajawahi kupata shida ya umeme na wala hawajui adha ya mgao wa nishati hiyo.
Anasema kuwa, licha ya kufaidika na nishati hiyo, hata mazingira ya eneo hilo hususan vyanzo vya maji vinatuzwa na kila mtu.
“Hata ukimwona mtu anakata jani la mti unamwangalia mara mbili, kila mmoja anajua maji yakikauka hakuna umeme. Kwa hiyo watu sasawanatunza mazingira sana,” anasema.
Wataalamu wa ATC wanasema kuwa, mtambo kama huo unaweza kufungwa kwenye taasisi kama shule ama chuo na una uwezo wa kuzalisha umeme wa kutosha.
Kitaalamu wanasema kwamba, wingi wa maji katika eneo husika ndiyo utakaokuza wingi wa umeme utakaokuwa unazalishwa.
Historia ya chuo
Mchakato wa kuanzisha Chuo cha Ufundi cha Arusha, ulianza mwaka 1970, baada ya Serikali ya Tanzania kuomba msaada kutoka Serikali ya Ujerumani.
Serikali ya Ujerumani kwa kupitia shirika lake la “German Agency for Technical Cooperation” ilikubali kujenga Chuo cha Ufundi Tanzania.
Pamoja na Serikali ya Ujerumani kukubali kujenga chuo hicho, uamuzi wa kujenga chuo hicho mjiniArusha ulifikiwa mwaka 1973/4 na mwaka 1975 ujenzi ulianza rasmi.
Mwaka 1978 majengo yote muhimu pamoja na vifaa vya kufundishia vilikuwa vimeshajengwa na kufungwa tayari kwa masomo na chuo kikapewa jina la “Technical College Arusha” (TCA)
Mei 1978 chuo hicho kilidahili wanafunzi 120 ambao walianza kusoma programu mbalimbali na Mei 1981 kilitoa wahitimu wake wa kwanza.
Tangu kuanzishwa kwake, chuo hikikimedahili maelfu ya wanafunzi kwenye ufundi wa aina mbalimbali wengi wao kwa sasa ni makandarsi wakubwa nchini.
Kutokana na kutambua michango yao, baadhi wamekuwa wakipata kazi ya kujenga hata majengo makubwa ya chuo hicho.

CHANZO: MWANANCHI
 
Chezea TCA wewe.... Hongera Mhandisi kwa kazi nzuri. Mkuu w Chuo pia hongera zake kwa kukubali vitu kama hivi vifanyike. Hapo naona matunda ya Hungury, si Prof. Sarungi peke yake.

logo.png
 
Back
Top Bottom